Breaking News

BONDIA AMIR MATUMLA KUZICHAPA NA AMAVILA WA NAMIBIA

Na Neema Mpaka - Bondia Amir Matumla anatarajia kupambana na bondia kutoka Namibia Paulus Amavila katika pambano lisilokuwa la ubingwa la Knockout ya Mama msimu wa tatu litakalofanyika Februari 28, mwaka huu Dar es Salaam.

Akitangaza mapambano ya Knockout ya Mama Dar es Salaam Leo Mkurugenzi wa Mafia Promotion Ally Zayumba amesema pambano hilo litakuwa la raundi nane uzito wa super weight.

Amesema anatarajia bondia huyu ambaye ni mtoto wa bondia wa zamani Rashid Matumla atafanya vizuri kwani ana hamu ya kufika mbali.

"Tumekaa naye tumezungumza naye na moja ya malengo yake alituambia tumtafutie pambano la kimataifa kwa hiyo litakuwa pambano lake la kwanza kwake la kimataifa,"amesema.

Zayumba amesema lengo la pambano hilo ni kuendelea kumsapoti Rais Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa ni mwanamichezo namba moja hivyo, watatumia pambano hilo kuendelea kutangaza mazuri aliyofanya.

Kwa upande wake Amir amesema:" Nashukuru sana Mafia kwa kunipokea, naahidi Watanzania nitaendeleza kwa ukubwa zaidi, sasa hivi naendelea na mazoezi, watu waje kwa wingi watafurahi zaidi

Kutakuwa na jumla ya mapambano 12 kati ya mabondia wa ndani na nje ya nchi. Na miongoni mwao yumo Abdallah Pazia 'Dula Mbabe', Oscar Richard na Yohana Mchanja.

Awali, Zayumba alitaja viingilio kuwa ni sh 50,000, 20,000 na sh 10,000.

Mwanamuziki Nurdin Bilal 'Shetta' amesema mabondia hawana budi kutumia nafasi hiyo waliyopata kujitangaza na kujiondoa katika hali mbaya ya kiuchumi kutoka chini kuwa juu.

 Aidha amesema anamshukuru Dr Samia Suluhu Hassan rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa hamasa na support kubwa anayoitoa kwa mabondia wa Tanzania.
 

No comments