MSTAAFU PINDA: VIJANA CHANGAMKIENI MAFUNZO YA VETA

Na Neema Mpaka, Dar es salaam - Vijana nchini wametakiwa kutumia fursa ya kujiunga na vyuo vya mafunzo ya ufundi,(VETA) ili kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamesemwa Leo jijini dare es salaam na waziri mkuu mstaafu mheshiwa Mizengo Peter Pinda alipokuwa akitembelea mabanda yaliyoandaliwa na vyuo vya ufundi (VETA) katika kuendelea kuadhimisha miaka 30 ya VETA.

Amesema vijana watumie nafasi ya kupata maarifa ya ufundi wa veta ili kujikimu katika maisha Yao ya baadaye.

"Vijana wapate nafasi kupata maarifa ya ufundi stadi kupitia kwenye vyuo vya veta vya serikali na vya watu binafsi, makampuni binafsi ili mradi wametolewa ufafanuzi na watu wa veta kuwa vyuo hivyo binafsi na kampuni vinafaa." Alisema mhe. Pinda.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore amesema mheshimiwa Pinda amekuwa mdau mkubwa wa veta na ni mshauri na alisimamia matokeo na maboresho ambayo yametokea veta mpaka hivi sasa

Aidha amesema ujuzi ni kwa kijana yeyote wa kitanzania ambaye anatakiwa aweze kupata na kufanya shughuli mbalimbali hapa nchini.

Wakati huo huo CPA Kasore amesema kilele Cha maadhimisho ya miaka 30 yanatarajiwa kumalizika tarehe 20 march 2025.

No comments