SHEIKH JALALA AONGOZA MATEMBEZI YA AMANI YA SIKU YA KIMATAIFA YA QUDS, ASISITIZA AMANI, UMOJA NA MSHIKAMANO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

Kiongozi mkuu wa dhehebu la shia Ithnasheriya Sheikh Hemed Jalala akizungumza mara baada ya matembezi ya amani ya siku ya kimataifa ya QUDS ambayo ufanyika kila ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa ramadhani 

Dar es salaam - Kiongozi mkuu wa dhehebu la shia Ithnasheriya Sheikh Hemed Jalala amewaongoza waislam na waumini wengine wa wa dini mbalimbali katika matembezi ya amani ya siku ya kimataifa ya kupinga manyanyaso, dhulma na mateso dhidi ya wapalestina yanayofanyika kila ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa ramadhani.

Akizungumza na umma wa washiriki wa matembezi hayo shekh jalala amesema zaidi ya karne na karne sasa tangu dunia ianze kushuhudia mgogoro kati ya wa Israel na Palestina juu ya umiliki wa ardhi ya taifa la Palestina, pamoja na jitihada za kuutatua mgogoro huo ikiwemo kurekebisha mipaka ya ardhi kushindwa kufikia muafaka.
"Siku hii adhimu nyenye lengo la kuenzi na kupaza sauti juu ya amani, umoja na mshikamano kwa uislam na wasio waislam pamoja na kukumbuka madhila yanayoendelea duniani kote hususani katika ardhi ya Palestina " Alisema Sheikh Jalala.

Alisema siku Quds ni siku ambayo inawaleta pamoja waislam na wakristo pia ni siku ya kukumbuka madhila wanayoyapata taifa la palestina.

Sheikh Jalala aliongeza kuwa siku hii imekuwa ikiubili na kutangaza juu ya kuleta umoja kati ya waislam na wakristo , waislam na wayahudi kutokana na kukusanya dini zote pamoja na kupaza sauti kuimiza umoja, hasa katika ardhi ya Palestina katika mji wa Yerusalem mambapo ndio makao makuu ya dini zote mbili.
Aidha Sheikh Jalala ametumia matembezi hayo kutoa wito pia kwa watanzania Kuendelea kuilinda na kuienzi tunu tulionayo ya amani, umoja na utulivu hususani mwaka huu tukielekea katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

"Nitoe rai kwa watanzania kuendelea kulinda tunu tuliyonayo ya amani, umoja na shikamano kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika badae mwaka huu ili tuweze kuchagua viongozi wetu kwa amani na itulivu". Alisema Sheikh Jalala


No comments