CRJE YAJIVUNIA KUENDELEA KUTOA UJUZI KWA WAHANDISI WAZAWA

Urafiki wa Tanzania na China: CRJE yajivunia kuendelea kutoa ujuzi kwa wahandisi wazawa


Na Mwandishi Wetu Kampuni ya CRJE (East Africa) Limited kutika China ambayo imekuwa nchini kwa zaidi ya miaka 50 ikidukisha urafiki mkubwa kati ya nchi hizi mbili imesema inajivunia kuona ikiendelea kutoa ujuzi kwa wahandisi wazawa katika sekta ya ujenzi. Katika viwango vya kimataifa, Kampuni ya CRJE ni mkandarasi mwenye ubora wa nyota tano.

CRJE (East Africa) Ltd ina wafanyakazi zaidi ya 5,000 katika nchi za Afrika Mashariki.

Kampuni ya CRJE imeshajenga jumla ya mita za mraba milioni 3 nchini Tanzania ndani ya miaka 50, ikijumuisha zaidi ya miradi 30 ya kihistoria kama vile Daraja la Nyerere, Chumba Kipya cha Mijadala ya Bunge Dodoma, Kituo cha Mikutano cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Dodoma, jengo la Rita, Uhuru Heights na Nyerere Foundation Square nk.

Kampuni ya CRJE ndiyo yenye rekodi ya kasi zaidi kwa ujenzi Afrika Mashariki ambapo ina rekodi kwa ya kumaliza sakafu moja ya kawaida ndani ya siku sita. Rekodi nyingine ya kampuni ni kukamilika kwa usanifu na ujenzi wa Kituo cha Mikutano cha Dodoma ndani ya miezi 7, na kutengeneza kasi maarufu ya “Dodoma Speed”.

Kampuni pia imejenga hoteli nyingi za kiwango cha kimataifa za nyota tano nchini Tanzania zikiwemo hoteli ya Serengeti Four Seasons na hoteli ya Zanzibar Park Hyatt.

Daraja la Mwalimu Nyerere na miradi mingine mingi mikubwa imekuwa alama nzuri zaidi ya biashara ya kampuni hiyo. Kwa mtindo ubora wa kazi, sifa nzuri na miradi ya hali ya juu, ambapo kampuni imetunukiwa mara tatu ya "Mkandarasi Bora wa Kigeni" nchini Tanzania, na mara mbili "Tuzo ya Luban" tuzo ya Oscar ya China kwa ubora katika ujenzi.

No comments