WAFANYABIASHARA WADOGO WAPIGWA MSASA MATUMIZI YA MTANDAO KUTUNZA TAARIFA ZAO

Na Neema Mpaka, Dar es salaam - Serikali imesema itashirikiana na wafanyabiashara wadogo wadogo kuhakikisha kwamba wanapewa elimu ya manufaa ya tovuti (website) ili kumsaidia mfanyabiashara Kujua taarifa zake za biashara na Kujua masoko ya biashara.

Hayo yamesemwa Leo jijini dare es salaam na afisa biashara mkuu ofisi ya mkuu wa mkoa wa dare es salaam Ndugu Thabiti Martha wakati wa uzinduzi wa tovuti (website) ya jumuiya ya vikundi vya wenye viwanda na biashara ndogo ndogo Tanzania ( VIBINDO SOCIETY).
Aidha amesema watashirikiana na VIBINDO kupitia maafisa biashara wa wilaya, maafisa maendeleo ya jamii wa wilaya kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wadogo wote wanafahamu uwepo wa tovuti website hiyo na wanajisajiri na wanatumia kwa madhumuni yaliyokusudiwa ya kukuza biashara zao.

"Kama mlivyoona kwenye uzinduzi wa Leo wa tovuti (website) wafanyabiashara wa VIBINDO wamewaalika wafanyabiashara wadogo wadogo wenzao, wanaoitwa KAWASO, jumuiya ya wafanyabiashara wa karikoo, machinga hao wote tutashirikiana kuhakikisha wanapewa elimu ya manufaa ya website hiyo"Amesema Thabiti.

Aidha amesema lengo la uzinduzi wa website hiyo ni kusajili na kumsaidia mfanyabiashara mdogo mdogo na sio kutoza Kodi Bali kumsaidia kuingiza taarifa zake na yeye pia kupata taarifa za biashara nyingine ili kukabiliana na ushindani katika masoko ya biashara.
Kwa upande wake wenyekiti wa jumuiya ya vikundi vya wenye viwanda na biashara ndogo ndogo Tanzania (VIBINDO SOCIETY) Ndugu Gastone Kikuwi amesema website hiyo itawasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo kuwa na maeneo salama ya kufanyia biashara, kupata huduma za mitaji, huduma za hifadhi ya jamii, kupata mafunzo yanayolingana na shughuli zao, lakini pia waweze kulipa Kodi zinazostahiki.

Naye mratibu mkuu wa miradi kitaifa anayefanyakazi na shirika la kazi duniani ( lLO) bi Glory Blasio amesema shirika la kazi duniani limefanya kazi kwa karibu na VIBINDO ikiwa ni sehemu ya kazi ambayo shirika la kazi duniani linafanya kuhamasisha urasimishaji wa biashara hasa biashara ndogo ndogo na za kati.

No comments