NCCR MAGEUZI YAMTEUA HAJI AMBAR KHAMIS MGOMBEA URAIS 2025
Na Mwandishi Wetu, Dodoma - Chama cha NCCR Mageuzi kimetangaza kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu 2025 na hakitambui kitu kinachoitwa ‘No Reform, No Election’.
Akizungumza katika mahojiano mara baada ya kutangazwa na Mkutano Mkuu wa chama hicho leo 29 Machi 2025 mjini Dodoma kumtangaza Haji Ambar Khamis kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho, alisema wanashiriki uchaguzi mkuu kikamilifu.
Alisema suala la uchaguzi mkuu ni la kikatiba na mtu yeyote akivunja katiba ni uhaini na wao NCCR Mageuzi hawapo tayari kufanya hivvyo.
“Hatupo tayari kuvunja katiba ya nchi wala ya chama na hata hayo maendeleo utayadai vipi kama usiposhiriki uchaguzi mkuu?” alihoji,
Joseph Selasini, ambaye amechaguliwa kuwa mgombea Mwenza alisema anasikia kuna watu wanasema “No Reform, No Election” wao NCCR Mageuzi hawaelewi.
“Hatuelewi, wala hatujaelimishwa hivyo tutaendelea kuhubiri uchaguzi mkuu” alisema Selasini.
Post Comment
No comments