JESHI LA POLISI KANDA MAALUM KUIMALISHA ULINZI KUELEKEA SIKUKUU YA EID AL-FITRI

Dar es salaam - Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewataka wazazi na walezi kuwa makini na kutowaacha watoto kwenda katika kumbi za burudani na maeneo mengine pasipo kuwa na uangalizi maalum kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea watoto kupotea, kupata ajali au kufanyiwa vitendo vinavyoweza kuhatarisha afya na maisha yao.

Akizungumza mapema leo Machi 30, 2025, Jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,SACP Muliro Jumanne Muliro amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wamejipanga kuhakikisha kuwa linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi chote cha sikukuu. 

Amesema jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam kwa kutambua kuwa tarehe 31, Machi 2025 au Aprili 1,2025 kutakuwa na sikukuu ya Eld-al-fitri kutegemea kuandama kwa mwezi. Kutokana na umuhimu wa sikukuu hiyo, suala la ulinzi na usalama limewekewa uzito mkubwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji ikiwa pamoja na fukwe za bahari ili sikukuu hiyo isherehekewe kwa amani na utulivu.

Kamanda muliro aliongeza Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa dalili za vitendo vyovyote vya kijinai au vile vya usalama barabarani kwa madereva wote wa vyombo vya moto wenye tabia ya kupuuza na kukiuka sheria na usalama barabarani

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limetlfanikiwa kumkamata EliaAsule Mbugi @ Dogobata Mnyakyusa (25), mkazi za Segerea dereva aliyekuwa aliendesha gari namba T 580 EAE aina ya TATA @ Dajadala ambaye alitoroka Machi 17,2025 mara baada ya kusababisha ajali iliyosababisha kifo cha SP Awadh Ramadhani Chico aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya kipolisi Chanika.

"Mtuhumiwa alikamatwa na makachero wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam tarehe Machi 27, 2025 maeneo ya Mbalizi Mkoani Mbeya, na taratibu zote zimekamilika atafikishwa mahakamani haraka iwezekenavyo kujibu tuhuma zinazomkabili". Alisema SACP Muliro.

No comments