WAUMINI WA DINI YA KIISLAAM  MKOANI TANGA  WATAKIWA KUYAISHI YALE WALIYOJIFUNZA  KATIKA MWEZI MTUKUFU  WA RAMADHANI

TANGA - Wumini wa dini ya Kiislam  na Watanzania  kwa ujumla  wametakiwa kuyaishi yale waliyojifunza ndani ya Mwezi mtukufu wa Ramadhan ikiwa ni pamoja kujenga tabia ya kuwa na hofu ya Mungu.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti  wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) Mkoa wa Tanga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,  Rajabu   Abdulrahman wakati akitoa salamu zake kuelekea  Sikuku  ya Iddi  el Fitri ambayo inatarajiwa kuswaliwa  Machi 31 mwaka  huu sawa na Mwezi Mosi Shaawal mwaka 1446.

Aidha Rajab  Abdulrahmana amewapongeza wafanyabiashara wa Mkoa  wa Tanga kwa kuuheshimisha mwezi wa Ramadhan kwa kutopandisha bei za bidhaa zao  tofauti na miaka mingine .

"Niwapongeze sana wafanyabiashara wa Mkoa wa tanga bei za bidhaa ukiangalia kwa upatikanaji wake kabla ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na ndani ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani  bei ni zile zile kwa hiyo tunawashukuru na tunawapongeza na tunapokwenda kuimaliza ibada hii ya mwezi mtukufu wa Ramadhani nipende kuwaasa sana wana Tanga wenzangu tuendelee kuishi kwa namna ambavyo Mwenyezi mungu (S.W) ametuamrisha, tuache yale yote Mwenyezi Mungu ametukataza na hiyo maana halisi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani" amesema Rajabu  Abdulrahman.

Katika hatua nyingini mwenyekiti huyo wa CCM  Mkoa amewataka wakazi wa Mkoa Tanga kuendelea kudumisha amani, upendo,Umoja na Mshikamano  huku akionya wale wale wote wenye nia  ovu ya  kupanga ama kujaribu kuleta vurugu ndani mkoa wa Tanga.

"Tusikubali waje watu waturubuni kwa maneno ya kisiasa, waje watu waturubuni kwa nama wanavyojua wao wenyewe kwa waliowatuma kuvunja amani ndani ya mkoa wetu wa Tanga,Tumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Rais amejipambanua wazi katika suala zima la amani wenye kuichezea amani hana msalie Mtume kwa sabababu tunajua madhara yake " amesema  Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Tanga  Rajab Abdul Rahman.

Mbali na hayo Rajab Abdulrahman amewataka wakazi wa Mkoa  wa Tanga  kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa na afya njema ili aweze kuwatumikia Watanzania. 

No comments