TAASISI YA JAMII KWANZA INITIATIVE YATOA MKONO WA EID EL FITR KWA WENYE UHITAJI DAR

Dar es salaam - Taasisi ya isiyo ya Kiserikali ya Jamii Kwanza initiative (JKI) kwa Kushirikiana na Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Amani Kata ya Kipunguni, Ilala Jijini Dar es salaam Leo Machi 29, 2025 imefanikisha kutoa mkono wa Iddi kwa watu wenye uhitaji wakiwemo Yatima na Wajane ili waweze kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitri inayotarajiwa siku ya Jumatatu inategemea na kuandama kwa mwezi.

Akizungumza mara baada ya kugawa sadaka hiyo Mkurugenzi wa JKI Daniel Migera amesema kuwa kitendo walichokifanya ni moja ya jukumu lao kama Taasisi kurejesha kwa Jamii shukurani na kudumisha amani,upendo na furaha.
"Tumeamua kunyoosha mkono ili kudumisha amani na Umoja,tumetoa swadaka hiyo ili Kuwawezesha na wao kufurahia hii muhimu kwao mara baada ya kumaliza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani " Amesema Migera.

Bw. Migera ametoa Rai kwa Taasisi zingine wakiwemo Wadau mbalimbali, watu wenye Uwezo kuwasaidia wenye uhitaji Maalum kwani kufanya jambo kama hilo ni muhimu kwa kujenga amani,Umoja, mshikamano na furaha kwenye Jamii.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo, Abdi Hashim Mahanyu ameishukuru JKI kwa kuwaunga Mkono na kufanikisha kuwapa mkono wa Idd Watoto Yatima,Wajane na wenye uhitaji kwa kuwapa chakula ili waweze kufurahia siku ya Sikukuu.
Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Kivule Mashabiki na Mdau mkubwa wa JKI ameishukuru Serikali ya Mtaa huo kwa kukubali Kushirikiana na Taasisi yake na kuona umuhimu wa kuwakimbilia wenye uhitaji na kuongeza kuwa kitendo hicho ni suala la kiimani na Katika mafundisho ya dini zote mbili lipo la kuhurumiana na kupendana.

Mmoja ya wakina - Mama waliopewa swadaka hiyo Jamila Ally ameishukuru Taasisi hiyo ya JKI pamoja ofisi ya Serikali ya Mtaa wao kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia na kuweza kuwapa Sadaka hizo.
Katika Mfungo huu tumeona viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakitoa sadaka kwa Makundi ya watu mbalimbali ikiwa ni katika kufanya matendo mema katika mwezi huu, Ambapo Waislam na Wakristo wamefunga kwa Pamoja.


No comments