PBZ BANK YAFUTARISHA WATEJA WAKE DAR

Mkurugenzi Mwendeshaji wa PBZ Bank, ndugu Arafat A Haji akiwa na Meya wa jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto na Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam Walid Alhad Omar katika Iftar ya pamoja na wateja wetu iliyoandaliwa na PBZ Bank leo tarehe 17 Machi 2025.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa PBZ Bank, ndugu Arafat A Haji, akiwasili Johari Rotana Hoteli, Dar es Salaam kushiriki Iftar ya pamoja na wateja wetu iliyoandaliwa na PBZ Bank leo tarehe 17 Machi 2025.
Mshindi wa Pili wa Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur an yaliyofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jana tarehe 16 machi 2025, Abdulmuhaimin Mohamed Jumaa kutoka Libya ameifungua kwa dua Iftar iliyoandaliwa na PBZ Bank kwa wateja.


Dar es salaam - PBZ Bank katika kukamilisha moja ya nguzo muhimu ya mwezi mtukufu wa ramadhani imwafutarisha wateja wake leo tarehe 17 Machi 2025 katika Hoteli ya Johari Rotana, Dar es Salaam.

Akizungumza katika mara Baada ya Iftar hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa PBZ Bank, ndugu Arafat A. Haji amewashukuru wateja wetu kwa kujumuiaka nasi katika Iftar hiyo ya pamoja.
Pia kwa umuhimu, ndugu Arafat amesema PBZ Bank imefanya maboresho makubwa ya huduma zake ikiwa ni pamoja na kufungua matawi zaidi bara na visiwani kwa lengo la kusozeza huduma zake karibu zaidi kwa jamii.

"Nichukue nafasi hii kuwakaribisha wakaazi wa Dar es slaam na Watanzania kwa ujumla kuitumia huduma bora zinazotolewa na PBZ Bank kwani huduma zake ni nafuu na bora zaidi". Alisema Bwana Haji



No comments