DKT. JAFO AFUNGUA MAONESHO YA NNE MKOA WA PWANI YA BIASHARA VIWANDA NA UWEKEZAJI ATAKA YAWE YA KITAIFA
KIBAHA - Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo ametoa maagizo kwa Katibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha kuwa maonesho ya Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Pwani yanakuwa maonesho ya kitaifa kwa kushirikiana na mkoa wa Pwani Katika kuandaa maonesho hayo kila mwaka kuanzia Mwakani 2025,
Akizungumza wakati akifungua maonesho ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji yanayofanyika Kibaha mkoani Pwani Katika viwanja vya Maonesho hayo kibaha meli moja
Hata hivyo ametoa wito kwa Watanzania kupenda bidhaa zinazozalishwa nchini ili kusaidia kukuza sekta ya uwekezaji, pamoja na kuzitaka taasisi zinazojihusisha na masuala ya biashara na uwekezaji kuhakikisha zinaweka jitihada kwa kuwa wawezeshaji badala ya kukwamisha katika mchakato wa kuanzishwa kwa Viwanda na uzalishaji bidhaa.
"Nitoe WITO kwa watanzania wakati wa Kupenda bidhaa zetu ni Sasa maana zinazalishwa kwa viwango na Teknologia ya kisasa ambazo zinakizi masoko ya kimataifa kama Ulaya, Amerika, Asia nk" alisisitiza Dkt Jafo
Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge ameeleza kuwa mkoa unatarajia kuongeza viwanda kwa asilimia 30 ili kuendelea kuchangia kukuza zaidi sekta ya uwekezaji nchini kutoka Pwani,
Mkoa wa Pwani una jumla ya viwanda 1533, ambapo zaidi ya viwanda vipya 131 vimejengwa kwa kipindi cha miaka minne na haya ni Maonesho ya NNE tokea kuasisiwa kwake,
Hata hivyo aliwataka uwongozi wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe kutangaza Eneo la Uwekezaji wa Viwanda la Visegese industry Park lililopo kata ya kazimbubwi,
Kauli mbiu ya Mwaka 2024 "PWANI SEHEMU SAHIHI YA UWEKEZAJI"
No comments