MSIGWA: MIRADI ILIYOSAJILIWA NA TIC TANGU 2021 IMELETA AJIRA LAKI 5
Pwani - Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema katika kipindi cha miaka minne ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani miradi 2099 imefanyia nchini katika kipindi cha mwezi Machi 2021 hadi February 2025.
Akizungumza katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika katika eneo la Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Kibaha Vijijini mkoani Pwani siku ya Jumapili Machi 16, 2025 amesema serikali imeweza kuongeza isajili wa miradi mbalimbali nchini.
"Katika kipindi cha miaka minne ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kati ya mwaka 2021 Machi hadi Februari 2025, tumefanya uwekezaji wa miradi 2099 ambayo imesajiliwa kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)". Alisema Msigwa
Alisema Miradi hii imetuletea jumla ya ajira 53,9488 ambazo zimezalishwa kutokana na uwekezaji huu, sasa mitaji iliyowekezwa ndani ya nchi ina thamani ya Dola za Marekani bilioni 25.098 ambazo ni sawa na Shilingi za Kitanzania trilioni 69 ambazo zimewekezwa kwa kipindi hiki.
Kwa upande wa miradi mipya ambayo imeanzishwa amesema jumla miradi mipya 1982, ambapo miradi ile 2099 ya kwanza niliyokutajieni ni miradi ambayo imesajili.
Aidha Msigwa aliongeza kuwa Katika miradi hiyo mipya kuna miradi ya ubia miradi ya ubia 476 ambayo Watanzania wanashirikiana na wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali duniani, kwa upande wa miradi iliyohusisha upanuzi wa maeneo ni miradi 117, lakini pia ipo miradi ya Watanzania ambayo tayali imesajilia ni 719
Post Comment
No comments