BANDARI KAVU YA KWALA KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MIZIGO BANDARI YA DAR - MSIGWA
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Serikali imeamua kuwa na Bandari kavu ya Kwala Mkoani Pwani hatua madhubuti ambayo serikali imechukua kupunguza msongamano wa Mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kufuatia hatua Serikali imesema uwekezaji Mkubwa zaidi ya Shilingi Trilioni 1 katika Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Msigwa ameyasema hayo leo, Machi 16, 2025 katika Mkutano wake na waandishi wa Habari Kwala Mkoani Pwani amesema wameona Bandari ya Dar es Salaam imelemewa hivyo imeona ni vyema kuwa na Bandari Kavu ya Kwala.
"Hatua madhubuti ambayo serikali imeamua kuzichukua kupunguza msongamano wa mizigo katika Bandar yetu ya Dar es Salaam , Tumefanya uwekezaji Mkubwa zaidi ya shilingi Trilioni 1 katika Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, Sasa tumeanza kupata Presha kubwa ya watu tutahifadhi mizigo baada ya kutoka Melini, Eneo la Dar es Salaam peke yake linakuwa lina lemewa sasa Serikali imekuja na Utaratibu wa Bahari kavu tumeijenga hapa Kwala ni hili eneo ambalo mnaliona hapa," amesema Msigwa.
Msigwa amesema eneo hilo limesakafiwa hekari 10 na kitu eneo ambalo ni kubwa na limezungushiwa hekari 60 huku eneo lote likiwa na hekari zaidi ya 120 ambazo zitatumika hapo.
Aliongezakwa kusema kuwa kuna Nchi jirani ambazo wamezigawia maeneo kwaajili ya kuweka bandari kavu ili mizigo yao ikitoka Bandari ya Dar es Salaam ipelekwe Kwala na baadae kuendelea na safari ya kwenda kwenye nchi zao bila kikwazo chochote.
"Tunafanya hivi kwasababu tunaamini bandari ni lango la Biashara na ni lango la Uchumi, tukifanya vizuri kwenye eneo la Bandari tutapata fedha nyingi ambazo zitatusaidia katika maendeleo ya Watanzania," amesema Msigwa.
Post Comment
No comments