TUNATARAJIA KUTOTEGEMEA BIDHAA ZA NJE KWA UWEKEZAJI WA VIWANDA NCHINI - MSIGWA
Pwani - Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Sekta ya viwanda ndiyo sekta inayoongoza kwa uwekezaji nchini, na katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi Februari 2025 nchini.
Akizungumza katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika katika eneo la Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Kibaha Vijijini mkoani Pwani siku ya Jumapili Machi 16, 2025.
Msigwa amesema jumla ya miradi ya viwanda 951 imesajiliwa, miradi ambayo inatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 12,4339 na huku uwekezaji mitaji ni Dola za Kimarekani bilioni 10.5 ambayo ni sawa na Shilingi trilioni 27, huo ndio kwenye viwanda. Alisema Msigwa.
Alisema Mitaji ya viwanda imechukua asilimia 42 ya mitaji yote ya sekta iliyosajiliwa katika kipindi hicho na kufanya miradi ya viwanda kuwa sekta inayoongoza katika sekta zote za miradi, mitaji na ajira.
Mfahamu kuwa eneo hili la viwanda , ukuaji wake ukilinganisha na miaka iliyopita hivi sasa tumeona umekua sana, tafsiri yake ni kwamba, pamoja na mapato ambayo tunayapata lakini tunakwenda kufanya kazi kubwa ya kuiondoa nchi yetu katika utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
"Tunapoangalia ukuaji wa uchumi wa nchi na kulinda uchumi wetu, ni lazima tupunguze kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi, sisi ndio tuzalishe kupeleka nje ya nchi",. Alisema Msigwa.
Post Comment
No comments