FUNDI MBAO MBARONI KWA KUWABAKA WATOTO WAKE WAWILI
Fundi mbao, Japhet Lendiman (38)
mkazi wa Daraja Mbili, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, baada ya kubaka watoto
wake wa kike wa darasa la sita na kidato cha kwanza.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema kuwa polisi wanaendelea na
uchunguzi ili kubaini kiini cha tatizo hilo ni nini na kufuatiwa na hatua ya
kufikishwa mahakamani.
Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi
la polisi tangu Juni 6, mwaka huu na upelelezi unaendelea kubaini undani wa
tukio hilo.
Akimzungumzia mtuhumiwa huyo, mmoja
wa majirani wa eneo hilo la Daraja Mbili (jina limehifadhiwa) alidai kuwa mzazi
huyo amezoeleka kwa tabia hiyo mbaya mtaani kwao.
Alidai kuwa mtuhumiwa huyo
amezoea kubaka watoto wake mara kwa mara wakati mama yao akiwa kazini na kwamba
Mei 28 majira ya saa 9:00 alasiri alimbaka tena mtoto wake (Jina tumelihifadhi)
wa darasa la sita shule ya Msingi Daraja Mbili ndipo taarifa zilipoanza kuzagaa
mtaani.
“Siku hiyo ya tukio lililosababisha
mzazi huyo kukamatwa mtoto aliona sasa uvumilivu umefika mwisho, alikwenda kwa
mama mkubwa na kutoa taarifa jinsi baba yake anavyomwingilia na kueleza kuwa
anataka kunywa sumu ili afe,” alieleza jirani huyo.
Alisema baada ya maelezo hayo mama
mkubwa aliamua kuhoji watoto wote wa shemeji yake akiwemo mwingine wa umri wa
miaka 14 (jina limeifadhiwa) ambaye yupo kidato cha Kwanza Sekondari ya Felix
Mrema, alikiri kuingiliwa na baba yake tangu mwaka 2016.
Aliendelea kueleza kwamba mama yao
mkubwa ambaye ni muuguzi (jina limehifadhiwa ) katika moja ya hosptali mkoani
Arusha, aliamua kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa na Polisi.
No comments