HIKI NDICHO KILICHOTOKEA BUNGENI LEO WAPINZANI WALIVYOSIMAMA BUNGENI NA KUIMBA WANA IMANI NA MKAPA, KIKWETE
Bunge limezizima kwa makofi baada ya
hotuba ya mpango wa bajeti ya kambi rasmi ya upinzani.Wabunge wa upinzani
ndiyo wengi waliobaki ukumbini baada ya wengi kwenda kufuatilia ripoti ya
kamati ya pili ya Rais John Magufuli kuhusu usafirishaji wa makinikia.
Wabunge wamesimama na kuanza kuimba
huku wakipiga makofi, marais wa awamu zilizopita; Benjamin Mkapa na Jakaya
Kikwete wametajwa.
"Tuna imani na Mkaaapa...oya oya
oya
Mkapa kweeeli...kweli
Kweli, kweli, kweli Mkapa.
Tuna imani na Kikweeetee...oya oya
oya
Kikwete kweeli
Kweli, kweli, kweli Kikwete."
Wimbo huo umeimbwa baada ya Waziri
Kivuli wa Fedha na Mipango, David Silinde kulitaka Serikali kuileta bungeni
mikataba yote ya madini ili ijadiliwe.
No comments