TIB CORPORATE BENKI YATEKELEZA AGIZO LA RAIS MAGUFULI LA KUTOA HUDUMA SAA 24 BANDARI YA DAR
Benki
ya Kibiashara ya Serikali ya TIB
Corporate imenza kutoa huduma kwa masaa 24 za kukusanya kodi katika tawi Dogo la TPA kwenye Bandari ya Dar es salaam kutekeleza agizo la rais wa
jamhuri wa muungano wa tanzania Dkt John Pombe Magufuli la kuzitaka taasisi
zote zinazotoa huduma katika bandari ya Dar es salaam kuanza mara moja kutoa
huduma zao kwa masaaa 24 hili kuongeza ufanisi.
Akizungumza
leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Bwana Frank Nyabundege alisema kufatia Benki hiyo kutiliana saini na
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kwa
ajili ya kuunganisha mfumo wa malipo ya kodi ujulikanao kama TAXBANK huduma ambao utafanyika bandarini
hapo.
Alisema
hatua hiyo itawezesha wananchi wote kulipia Kodi za aina mbalimbali pamoja na
tozo za bandari kwani Benki hiyo imejipanga kuhakikisha inaleta ufanisi katika
kutoa huduma.
Aidha Bwana
Nyabundege aliongeza kuwa benki hiyo
imejipanga kupanua wigo zaidi na kuboresha utoaji huduma za kibenki katika
ukusanyaji wa kodi hivi karibuni
inatarajia kufungua matawi ya kutolea huduma katika Bandari ya Mtwara na Tanga pamoja
na zingine ndani na nje ya Nchi.
Pia amevitaka
vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi kutambua kuwa kwasasa
Benki hiyo imeanza kutoa huduma ya kulipia kodi katika Tawi Dogo la TPA lililopo ndani ya Bandari ya Dar es
salaam kwa saa 24 kwa lengo la kuwarahisishia wanachi kulipa kodi zao bila usumbufu.