ALIYEKUWA RAISI WA KOREA KUSINI AFIKISHWA MAHAKAMANI
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8qbeYvs92cIDs2tFMxHKonA_wxXqRi3o3DPQpOGHjid6MIZJCsen8cqEGzwV19bNxqjhxo2jn_joQFrKKWe2mKtcPOl4tz-NRYF-z0l-IJ1eOLZw-D_Cj_fPvbVEA-CodTSbnTFJZDdGC/s640/1.jpg)
Aliyekuwa
Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza
kujibu mashtaka yanayomkabili, tangu alipokamatwa mwezi Machi mwaka huu.
Mwanasiasa
huyo aliyeondolewa madarakani kwa kashfa nzito, anakabiliwa na mashtaka kadhaa
ikiwa ni pamoja na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na kuvujisha siri za
Serikali. Hata hivyo, Park aliyefikishwa mahakamani hapo na gari la magereza
akiwa amefungwa pingu mikononi alikana mashtaka yote dhidi yake.
Park
anatuhumiwa kushirikiana na rafiki yake, Choi Sonn-sil, kuchota fedha kinyume
cha sheria kutoka kwa makampuni makubwa ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kampuni
ya Samsung, kwa malengo ya kupata mrejesho wa faida ya kisiasa.
Choi
Soon-sil ambaye pia anakabiliwa na mashtaka alifikishwa mahakamani pamoja na
mwanasiasa huyo lakini pia alikana mashtaka yote dhidi yake.
Kiwango
cha juu zaidi cha adhabu kwa kosa la kupokea au kutoa rushwa nchini Korea Kusini
ni kifungo cha maisha jela.