KAULI YA SHY-ROSE BHANJI BAADA YA JINA LAKE KUKATWA NA KAMATI KUU YA CCM KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE AFRIKA MASHARIKI
Aliyekuwa
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Shy-Rose
Bhanji amelalamika jina lake kukatwa katika kinyang'anyiro cha kutetea nafasi
hiyo katika muhula ujao bila kuhojiwa juu ya tuhuma zilizopeleka jina lake
kukatwa.
Licha
ya malalamiko hayo, pia Shy-Rose Bhanji ametumia fursa hiyo kuwapongeza watu
waliochaguliwa kuwa wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki kupitia tiketi ya
Chama Cha Mapinduzi na kuwashukuru wabunge kwa kumpigia kura zilizomuwezesha
kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa mwanzo waliopata kura nyingi zaidi.
"Ingawa
jina langu limekatwa na Kamati Kuu ya Chama bila ya mimi nwenyewe kuitwa na
kuhojiwa ili nipewe haki ya kujibu hoja zozote dhidi yangu, nawapongeza wote
waliochaguliwa kuwa wagombea wa EALA kupitia CCM. Ninawashukuru sana Wabunge
kwa kunipigia kura nyingi zilizoniwezesha kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa
mwanzo walioongoza kwa kura" aliandika Shy-Rose Bhanji
No comments