DOYO HASSAN DOYO ATANGAZA RASMI NIA KUGOMBEA URAIS 2025

Morogoro - Katibu mkuu wa chama cha chama cha National League for Democracy (NLD) Mhe Doyo Hassan Doyo ametangaza rasmi nia ya kuomba ridhaa ya chama hicho kuwa mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia katika uchaguzi mkuu utakaofanyika badae mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Machi 14, 2015 mkoani morogoro amesema mara baada ya kutafakari pamoja na kushauriana na watu wake wa karibu hili kupata busara zao ikiwemo wazee kutoka ndani ya familia na nje ya nchi juu ya dhamira yangu na malengo yangu kwa taifa letu

“Watanzania wenzangu, nimeitikia wito wa taifa! Nimeitikia wito wa wazee wangu, familia yangu, na dhamira yangu ya dhati. Taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa na ninaamini kuwa nina uwezo wa kuongoza mageuzi haya,” alismea Mhe. Doyo 

Alisema uchaguzi huu ni wa sita tangu kirejeshwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini hivyo ni uchaguzi muhimu sana katika taifa letu na muhimu watanzania wakaelewa hivyo kwani ni Zaidi ya miaka 30 nchi yetu imekua ya kidemokrasia, pili ni haki yangu ya msingi ya kikatiba kuomba kugombea nafasi hii kubwa katika nchi yetu kwani nimejitathimini kifikra, kiuwezo na kiuweledi kuwa naweza kumudu nafasi hiyo,

Amevitaja baadhi ya vipaumbele vyake mbavyo amejipanga kuhakikisha kuwa ataanza kuvitekeleza pindi akipata ridhaa ya watanzania kuwaongoza kuwa ni Ajira, Elimu, Kilimo na ufugaji, Rasilimali za maji, Kuziba mianya ya ukwepaji wa kodi pamoja na kupambana na rushwa.

Amevitaja vipaumbele vingine kuwa ni Kujenga taifa la walipa kodi kwa kiwango kinachostahili, Kuweka nguvu katika sekta ya madini, Kuongeza jitihada kwa Watoto wa kike katika kupata elimu/Teknolojia, kuimarisha muungano wetu pamoja na kuboresha mazingira ya sekta binafsi ili kukuza na kuongeza tija na ufanisi wa utendaji wa shughuli za kiserikali na kijamii.

"Mnaweza kujiuliza kulikoni kuomba nafasi nyeti katika nchi yetu. Jibu ni kwamba bado naona kuna masuala makubwa na muhimu ambayo hayajafanyiwa kazi ipasavyo katika nchi yetu kama na ndio maana nimeamua kuja na vipaumbele hivi". Alisema Mhe. Doyo

Ikiwa chama changu cha National League for Democracy (NLD) kitanipitisha kugombea nafasi hii katika uchaguzi utakaofanyika octoba mwaka huu niwahakikishie kuwa nipo tayali kutoa ushindani kwa wagombea wa vyama vingine kwa kutangaza sera bora za chama chetu ili watanzania watuchague na kuweza kupata ridhaa ya kushika dola.

No comments