TATHMINI YA JUKWAA LA WAHARIRI WIKI MOJA YA KUSUSIA HABARI MAKONDA
Bodi ya Jukwaa la Wahariri
Tanzania (TEF) imekutana jijini Dar es Salaam leo Machi 30, 2017. Pamoja na
mambo mengine imejadili mwenendo wa vyombo vya habari ndani ya wiki moja tangu
tulipotoa msimamo wa kutotangaza habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda.
Bodi imepitia habari za Mkuu wa
Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa msimamo wa kumfungia. Bodi inapenda
kawapongeza wahariri wote waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha
habari za Mkuu wa Mkoa kwa wiki nzima.
Bodi inapenda kusisitiza kuwa
wahariri katika vyombo vya habari; magazeti, radio na televisheni waendelee na
msimamo wa kususia habari za Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, hadi atakapotimiza
takwa la kuomba radhi kwa tukio la kuvamia kituo cha Clouds.
Aidha, Bodi inatoa wito kwa
viongozi wa mitandao ya kijamii kuunga msimamo huu. Bodi inapenda kufafanua
kuwa Mhe. Makonda amewekewa vikwazo Maalum (Smart Sanction) kwa mikutano
atakayoiandaa au matukio atakayoyaongoza habari zake hatutazichapisha.
Wakati huo huo, kituo cha
Clouds kimepongezwa kwa kumsimamisha kazi mtangazaji aliyekiuka msimamo wa
kutotangaza habari za Makonda.
Bodi pia imewasiliana na
Uongozi wa UTPC na kukubaliana kwamba msimamo huu uendelee.
Theophil Makunga,
Mwenyekiti TEF
Imetolewa Leo,
Machi 30, 2017
No comments