ACT YAZINDUA OPARESHENI LINDA DEMOKRASIA LINDI

Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza wakati wa kongamano la viongozi mkoa wa Lindi lenye kauli mbiu ya operesheni linda demokrasia lililofanyika Lindi mjini, Machi 29, 2025.
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo bara, Issihaka Mchinjita akizungumza wakati wa kongamano la viongozi mkoa wa Lindi lenye kauli mbiu ya operesheni linda demokrasia lililofanyika Lindi mjini, Machi 29, 2025.


Lindi - Chama cha ACT  Wazalendo kimezindua rasmi Oparesheni linda Demokrasia ambayo itafanyika nchi nzima ili kukutana na wanachama pamoja na watanzania juu ya umuhimu wa kulinda Demokrasia na kupigania mabadiliko mbalimbali ya Uchaguzi.

Akizungumza katika Uzinduzi huo Kiongozi wa Chama Mstaafu Zitto Kabwe amesema ni umuhimu kuwa na tume huru ya uchaguzi ila kwa namna mchakato wa Sheria mpya ya Tume huru ilivyo patikana na mapungufu yake hayaifanyi tume hiyo kuwa huru hivyo kusisitiza mabadiliko ya mifumo mbalimbali ya uchaguzi na mabadiliko madogo ya katiba maana muda bado upo.

Alisema Sheria hiyo ambayo imepitishwa na asilimia kubwa ya wabunge wa CCM na kusainiwa na Mwenyekiti wa CCM ambae ni Rais lakini bado ni ngumu kuifuata.

Aidha zitto ameeleza umuhimu wa kupigania Demokrasia ili heshima ya Kura ya wananchi irudi na pia amewaeleza gharama inayo tokana na kupigania Demokrasia na kuwasihi kuto kata tamaa.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo bara, Issihaka Mchinjita amesema katika chaguzi tatu mfululizo thamani ya kura imepotea. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hakukuwa na kura, takribani wagombea wote wa upinzani walienguliwa. Mwaka 2020 tuliona kwa mara ya kwanza kura feki zikizagaa hovyo barabarani. Mwaka 2024 wakafanya kama mwaka 2020.

Alisema Matumaini yote tuliyokuwa nayo ya mageuzi kwenye uchaguzi na matarajio yetu yote kuwa mageuzi hayo yataaanza kutekelezwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, yameyeyuka, tumechapwa kibao kikali sana cha uso

"Wote ni mashahidi Tumewaona jinsi ambavyo taasisi zenye dhamana na wajibu wa kutulinda zikitumika vibaya katika uchaguzi uliopita 2024 wa vitongoji, vijiji na mtaa. Tujiulize, kama wanafanya kwa hao ambao hawatungi sheria yeyote itakuwaje kwa wabunge ambao wana madaraka ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais?". Alisema Mchinjika.
Alisema jukumu la Kulinda demokrasia ni wajibu namba moja wa kila raia. Raia wanapokosa uhuru wa kuamua nani awe kiongozi wao ni sawa na kuwa watumwa ndani ya nchi yao.

"Tunataka kuwa na Rais, Mbunge na Diwani ambaye anachaguliwa na kuwajibika kwa raia kama Mwakilishi wao. Tunataka Rais ambaye anajua amechaguliwa na raia sio na vyombo vya dola na kwamba uchaguzi ukifika atapimwa na raia kwa kazi zake". Alisema Mchinjika nakuongeza kuwa
"Hatuwezi leo baada ya miaka 60 ya uhuru, mtutu wa bunduki ndio uamue nani awe Kiongozi wetu. Mapolisi watuchagulie diwani, mbunge na Rais kiasi iwe tunajiuliza huyu Rais ni wa kwetu sisi raia au vyombo vya dola? Hatutaki kufika hapo"

Oparesheni Linda Demokrasia ni azimio la halmashauri Kuu ya ACT Wazalendo baada ya tafakuri kubwa ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa.



No comments