ARCHBISHOP MARK HAVERLAND AHAIDI USHIKIANO KWA ASKOFU MTEULE ELIBARIKI KUTTA
Mkuu wa wakfu na mhubiri Archbishop and Metropolitan, Mark Haverland akizungumza katika ibada ya kusimikwa rasmi Askofu mkuu wa kwanza wa kanisa la Aglikan katholiko nchini Elibaeiki Phillip Kutta ibada ambayo pia imeudhuliwa na Askofu wa Kanisa la Uamsho la Morovian nchini Emaus Mwamakula katika katika Viwanja vya Cathedral mlola
Mlola:
Mkuu wa wakfu na mhubiri Archbishop and Metropolitan, Mark Haverland amesema atashirikiana na Askofu mkuu wa kwanza wa kanisa la Aglikan katholiko nchini Tanzania, Elibariki Phillip Kutta katika huduma pamoja na kuhakikisha anatimiza maono yake katika kuiletea jamii maendeleo.
Akizungumza katika katika ibada ya kumsimika rasmi kuwa Askofu mkuu wa kwanza kanisa hilo nchini amesema amezunguka katika mataifa mengi duniani na kushuhudia mambo mengi lakini nimevutiwa na maono ya askofu Elibariki Phillip Kutta hususani katika kuhakikisha kuwa anawaletea pia maendeleo waumini wa eneo hili.
"Binafsi nimetembelea nchi duniani na kuonana na watu wengi ila nimpongeze askofu Elibariki Kutta kwa maono yake hasa swala la kuwaletea maendeleo mbalimbali kwa waumini wake hususani huduma ya maji na afya". Alisema Mkuu wa wakfu na mhubiri Mark Haverland.
Alisema Katika kipindi chote tangu kuwasili nchini ametembelea maeneo mbalimbali na kujionea jinsi ambavyo askofu Elibariki Kutta alivyo na maono makubwa na Nia ya dhati ya kutangaza neno pamoja na kutatua kero kero za waumini.
No comments