Breaking News

KONGAMANO LA KWANZA LA VIJANA WA KIISLAMU LAFANA

Taasisi ya ALFIRDAUS charitable foundation imefanya kongamano la kwanza la vijana wa kiislamu kufanyika nchini  lililowashirikisha vijana wa kada mbalimbali waume kwa wake mapoja na mashekh na wanazuoni.

Hafla hiyo ambayo ilienda sambamba na kutoa Tuzo za Tameya Awards kwa kutambua mchango yao katika kijamii na hata kiimani ambapo mgeni rasmi alikuwa shekh wa mkoa wa Dar es salaam, Shekh Walid ambaye alimwakilisha Mufti wa Tanzania Shekh Abubakari Zuberi.

Miongoni mwa vijana saba   (7) waliopata bahati ya kupata Tuzo  hizo katika hatua ya awali ni pamoja na Kassimu Mrisho, Omari Juma, Omari Baajuni , Ibrahim Omary , Ibrahim Hussein, Halima Shabuge na Azza Seleman
Akizungumza jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mwalimu Nyerere shekh Alhad Walidi amesema Tuzo hizo zinawaheshimisha vijana wa kiislamu kutambua majukumu yao katika kuendeleza dini ya mwenyezimungu.

“Tuzo hizi ni muhimu kwa ajili ya vijana wetu wa kiislamu kutambua amani na ushirikiano ni kitu muhimu, vijana ndio tegemeo kubwa la dini yetu ambapo mtume wetu Muhammad aliwasifu vijana na kuwajengea misingi Bora hivyo nasi tunawajibu wa kuwajengea vijana wetu kwenye misingi Bora,” amesema Shekh Walid

Aliendelea kusema vijana watumike vema katika umma wa kiislamu Ili kuwa wamoja katika kuimarisha dini yao na mambo yao ya msingi katika kuunufaisha umma wa kiislamu duniani kote.
Aidha Tuzo hizo za Tameya zililenga zaidi kwenye maeneo ya afya , kutangaza dini ya kiislamu , vijana kushirikiana katika masuala ya kijamii, biashara, kiteknolojia , sanaa na maadili mbalimbali.

Kwa upande wake Alfirdaus Chartable Foundation muandaaji wa tuzo hizo  amesema kuwa lengo la Tuzo hizo ni kuwapa fursa vijana wetu wa kiislamu wa moja katika kujisimamia dini yetu lakini kutoa fursa ya kujiendeleza katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.








No comments