KIKAO MAALUM CHA KAMATI TENDAJI FEMATA KUFANYIKA NOV 17 - 18 JIJINI DAR
TAARIFA MUHIMU KWA VIONGOZI WA KAMATI TENDAJI YA FEMATA, WACHIMBAJI, WAFANYABIASHARA NA WADAU WA MADINI TANZANIA
Tangazo Maalumu leo 09 Novemba 2024.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania FEMATA na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya FEMATA Mhe. John Wambura Bina, leo tarehe 09 Novemba 2024, anawatangazia Viongozi wa Kamati Tendaji ya FEMATA, Wachimbaji, Wafanyabiashara na Wadau wa Madini Tanzania; kuwa Kikao Maalum cha Kamati Tendaji ya FEMATA ambacho kilikuwa kifanyike tarehe 13 – 14 Novemba 2024 katika Ukumbi wa African Dream, Jijini Dodoma kimeahirishwa hadi tarehe 17 – 18 Novemba 2024.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Habari wa FEMATA Dr. Bernard Joseph, Kikao cha Kamati Tendaji sasa kitafanyika tarehe 17 – 18 Novemba 2024 katika Ukumbi wa Seashells Millennium Hotel, Makumbusho Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa FEMATA, mabadiliko ya Tarehe ya kikao hicho yamesababishwa na Mkutano Muhimu ya Kisekta (Tanzania Mining and Investment Conference 2024) utakaofanyika Jijini Dar es Salaam Tarehe 19 Novemba 2024.
Ambapo Viongozi na Watendaji wa Serikali ambao ni waalikwa kutoka Wizara ya Madini watakuwa Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi hayo.
Kwa kutambua umuhimu wa Viongozi na Watendaji wa serikali kushiriki katika mkutano huu muhimu, FEMATA inasikitika kuwajulisha kuhusu mabadiliko hayo.
IMETOLEWA NA KURUGENZI YA HABARI FEMATA - MAKAO MAKUU
No comments