WAZIRI MASAUNI: JESHI LA POLISI LIMEFANIKIWA KUPUNGUZA AJALI NA VITENDO VYA UHALIFU MWISHO WA MWAKA
Waziri Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Hamad Masauni akifafanua jambo katka mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kikao na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi kikao ambacho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri Sagini, Katibu Mkuu, Mmuya na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Wambura, kilifanyika Januari 4, 2024, D'Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Camillius Wambura akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari juu ya hali ya usalama matukio ya ajali na uhalifu katika kipindi cha mwisho wa mwaka 2023 kilifanyika Januari 4, 2024, D'Salaam.
DAR ES SALAAM
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Hamad Masauni amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hususani wananchi limefanikiwa kudhibiti vitendo vya ajali na uhalifu nchini.
Akizungumza jijini Dar es salaam mara baada ya kikao na viongozi wa ngazi ha juu wa jeshi la polisi nchi nzima wakiwemo Makamishna, wakuu wa vikosi na makamanda wa polisi amesema matukio ya ajali na uhalifu katika kipindi cha mwisho wa mwaka 2023 yamepungua ikilinganishwa miaka iliyopita.
Alisema mafanikio hayo yanakuja kufatia jitihada za jeshi la polisi nchini kwa kushirikiana na wadau mwengine ikiwemo wananchi jambo lilopelekea kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio hayo nchini.
"Jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau wengine tumefanikiwa kuimalisha hali ya usalama katika maeneo yote mwaka 2023, serikali itaendelea kuhakikisha kuwa hali ya usalama inaendelea kuimalika nchini" Alisema Waziri Masauni.
Alisema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha kuwa linachukua hatua matukio yote ya kiuhalifu ambayo yameripotiwa kutokea hivi karibuni nchini, hivyo amewataka wananchi kuwa na imani na jeshi hilo na pia kutoa ushirikiano pindi wanapoona vitendo au ishara yoyote ya uvunjifu wa amani.
Nae Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Camillius Wambura amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha kuwa linaendelea kudhibiti vitendo vyote vya kiuhalifu Nchini.
Akizungumzia kuibuka kwa vikundi vya vijana vinavyofanya uhalifu maarufu kama (panya road) alisema jeshi la polisi litaaendelea kukabiliana na vijana hao kulingana na nguvu watakayotumia na hawapo tayari kushuhudia askari wanakufa wakiwa wanapambana na vijana hao.
Alisema kuwa polisi hulazimika kufa kwa sababu za msingi pindi anapokuwa anatetea haki za raia, hivyo nguvu anayoitumia kumdhibiti mhalifu hutegemeana na nguvu ya mhalifu.
"Askari hawapaswi kufanya uzembe wa aina yoyote wanapopambana na vijana hao na wanapaswa kutumia nguvu ya kadri katika kuwashughulikia na kuwadhibiti". Alisema IGP Wambura.
Post Comment
No comments