Breaking News

PWANI NI SEHEMU SAHIHI KWA UWEKEZAJI, PAMOJA TUJENGE VIWANDA NA AJIRA- DR JAFO

Na Wazir Wazir, KIBAHA-PWANI
KATIKA muendelezo wa Maonesho ya Viwanda Biashara na Uwekezaji mkoa wa Pwani siku ya Nne 08.10.2022.

Akiongea wakati wa Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Pwani lilofanyika katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa katika Chuo Cha Uongozi Mwalimu Nyerere Mkoa Pwani lilohudhuriwa na Wakuu wa Mikoa ya Mtwara, Pwani na Pamoja na Wadau wa Biashara Mikoa ya Dar es salaam na Pwani na wafanya Biashara Mbalimbali Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Jafo aliunga mkono kauli mbiu ya Kongamano Kwa Kutoa Wito kusimamiwa Kwa Vitendo ili kuleta manufaa Zaidi kwa jamii na Serikali katika kukuza na kuinua Hali za wa wananchi kimaendeleo ya Uchumi,

Naunga mkono Zaidi Hii kauli mbiu ya Mwaka Huu 2022 ya Pwani ni Sehemu Sahihi Kwa Uwekezaji Pamoja Tujenge viwanda na ajira iwapo tukisimamia Kwa Vitendo tutapata faida Kubwa kiuchumi na kimaendeleo

Alisema Katika kuyafikia maendeleo ya Viwanda Pwani na Tanzania Kwa ujumla Daima tusiache kusimamia mazingira salama ya Watu na viumbe hai Kwa hiyo lazima Wakati wa uanzishwaji wake tupate kibali kutoka Wizarani Kwa muongozo Zaidi

"Nataka kusema Neno kwako mkuu wa Mkoa wa Pwani na Wakuu Wengine mliopo Hapa Kwa kuwambia Kongole Kwa kuandaa Kongamano na Maonesho Haya Viwanda Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Pwani na Hii ni Mara ya Tatu Ushauri kwangu muyaenzi na kuyaendeleza Kutafuta wawekezaji Ili kuinua Uchumi wa Taifa hongera Sana Ndugu Kunenge" alisema Dktt Jafo na luongeza kuwa 

"Uwekezaji Bado una nafasi Kubwa Sana Mkoa wa Pwani maana una madini Mengi mno ambayo yanaweza kukuza mapato ya ndani ya Halmashauri zetu kama Madini ya Misitu, Bahari, Mawe, Mifugo na Uvuvi na maji  Kwa ajili ya matumizi Mbalimbali iwapo ikitumika vyema Hii itakua Neema kwetu Kwa kizazi Cha Sasa na baadae hivyo naomba iendelee kutunzwa na kuhifadhiwa iwe Neema na sio Laana kwetu ikiharibiwa" alisisitiza Dkt Jafo

Mwisho Waziri Jafo alisisitiza kuendelea kuwaobea  Dua Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Makamu wake Pamoja na Mawaziri wote kunakotokana na kufanya Kazi ngumu na zenye kuhitaji Dua Kutoka Kwa wananchi wanaowahudumia 

"Ndugu zangu wa Pwani na Tanzania Kwa ujumla Tuendeleze ule Utamaduni wetu wa kuombeana Dua ya Kher Kwa Vingozi wetu wa kitaifa Hasa Rais na Makamu na Mawaziri wetu na Vingozi Wengine Kwa kufanya Kazi kutwa kucha Kwa maslahi ya Taifa alimazia Dkt Jafo,

Kauli mbiu ya Mwaka Huu ni PWANI NI SEHEMU SAHIHI KWA UWEKEZAJI PAMOJA TUJENGE VIWANDA NA AJIRA

No comments