Breaking News

IGP WAMBURA ATOA MAELEKEZO KWA RTO, WAKAGUZI WA MAGARI NA WATAHINI WA MADEREVA

Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camillus Wambura, amefanya  kikao na wakuu wa Polisi wa Usalama barabarani wa Mikoa yote Tanzania, wakaguzi wa magari na watahini wa madereva leo tarehe 21.02.2023 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.

Kikao hicho kimelenga kuwakumbusha mambo ya kuzingatia katika utendaji kazi, usimamizi, ufuatiliaji na kuona namna bora ya kuondokana na ajali za barabarani ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wa utoaji wa leseni za udereva.

Hii ni sambamba na kutoa mafunzo  kwa wakaguzi wa magari na watahini wa madereva wapya ambao watapewa  mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu.

Akiongea na waandishi wa wahabari katika kikao cha ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camillus Wambura amesema “Jeshi la Polisi  limefanya uchunguzi na kuona umuhimu wa kurekebisha mfumo wa utoaji wa leseni za udereva ili kudhibiti ajali za barabarani".


 

No comments