LHRC Yazindua Ripoti ya Makosa Yasiyo na Dhamana Jijini Dar
Timothy Marko
Kituo cha sheria na Haki za binadamu nchini (LHRC) kimeiomba Serikali kufanyia Marekebisho ya sheria ya utoaji wa Dhamana Kwa Makosa ya jinai ya Mwaka 1945.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Ripoti ya Makosa yasiyo na Dhamana Mkurugenzi wa kituo hicho, Bi Anna Henga alisema mchakato wa upatikanaji wa haki Kwa Makosa yasiyo na Dhamana unapingana na dhana ya kisheria ya ibara 13 (6) ya katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
"Katiba ya Mwaka 1977 ya Tanzania inayoweka dhana ya Msingi ya kutokuwa na hatia mpaka itakapo thibitishwa na mahakama, Dhana hii inalinda haki ya mtu yoyote kutendewa kama mwenye kosa la jinai kama mahakama hajaithibitisha kosa hilo kupia utaratibu maalumu". Alisema Bi Anna Henga.
Bi Henga alibainisha kuwa utafiti uliofanywa na kituo hicho ulieleza kuwa Sura namba 20 ya Makosa pamoja na sheria ya Uhujumu Uchumi na Sura namba 200 Kwa kuangalia vipengele vinavyo weka zuio la mtu kupata Dhamana.
"LHRC ilifanya utafiti wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura Na. 20 pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura Na. 200"
Alisema Utafiti ulifanya ulinganifu wa mfumo wa utoaji haki katika makosa ya aina hiyo katika nchi jirani za Kenya, Uganda, Malawi, Zambia pamoja na Zanzibar.
No comments