Breaking News

TIC Kuendelea Kushirikiana na Wafanyabiashara na Wawekezaji Kutoka Nje Ya Nchi Kukuza Sekta ya Biashara na Viwanda Chini

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Dkt Maduhu Kazi amesema kituo hicho kitaendelea  kushirikiana vizuri na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nje ya nchi kukuza sekta ya biashara na viwanda nchini.

Akizungumza mara baada ya kukutana na ujumbe kutoka  Jumuiya ya Afro - Asia (AFASU) ya nchini Misri ambayo imeasisiwa kwa lengo la kukabiliana na umasikini kwa kufanya biashara na uwekezaji 

Dkt. Maduhu alisema kuja kwa ujumbe huo nikutokana na matunda mazuri ambayo TIC ilifanya ziara Misri nakufanikiwa kuzungumza na wafanyabiashara na wawekzaji hivyo wamekuja nchini ili kuangalia mazingira ya Tanzania katika sekta muhimu za uwekezaji ikiwemo sekta ya Utalii wa fukwe.

"Sekta 16 muhimu zinatarajiwa kuwekezwa ikiwemo sekta ya Utalii, Kilimo, Elimu, Ufugaji wa Samaki, biashara na sekta zingine, hivyo ili kufanikiwa katika uwekezaji huo TIC itaendelea kutoa ushirikiano kwa wafanyabiashara wa Jumuiya hiyo." Amesema Dr. Maduhu.

Nae kiongozi wa Ujumbe huo ambaye pia ni raisi wa Jumuiya hiyo Dkt. Hossam Darwish alisema wameamua kuja Tanzania kuangalia mazingira ya uwekezaji hususani katika sekta ya Utalii wa fukwe, pamoja na kuweza kujenga kijiji cha utalii kitakachosaidia watu kupata mapumziko na famililia zao pamoja na vyakula vya asili.

"Huu ni mwelekeo wetu mzuri kujenga kijiji fulani cha mazao ya chakula lakini pia inakua kama utalii watu wanatembelea na familia zao nakupata mapumziko na chakula cha asili,kwenye jumuiya yetu kuna wawekezajj wakubwa ambao wanaweza kufanya utalii wa aina hii" alisema Dr. Darwish.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Mawasiliano, teknolojia ya Habari Dkt Jim Yonazi alisema kwasasa wanaamini kwamba ujumbe huo utasaidia kuendeleza sekta ya Viwanda na kukuza uchumi wa nchi.

Dkt. Yonazi aliongeza kuwa wizara yake inatarajia kufanya mazungumzo kwa lengo la kukuza sekta ya tehama nchi zetu yaani Misri na Tanzania kuendeleza mahusiano ya kiuchumi katika uwekezaji, ambapo masuala ya usalama mtandaoni yatapewa kipaumbele zaidi.


No comments