Breaking News

Watanzania Tangazeni Vivutio Vya Utalii

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) leo Septemba 18,2021 amefanya kikao na waandishi wa habari wa Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa maoni na kupanga mikakati ya kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania.

Akizungumza katika kikao hicho, amewataka Watanzania kuwa wazalendo kwa kuvitangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko nchini Tanzania, ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameonyesha kwa vitendo namna ya kutangaza vivutio vya nchi yake kupitia filamu maarufu ijulikanayo kama Royal Tour.

Aidha, Mhe. Masanja amesema kuwa Wizara yake itatengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya watalii watakaokuja ili waondoke wakiwa na mtazamo chanya kuhusu Tanzania.

Pia, Mhe. Masanja amewataka wawekezaji binafsi kujitokeza ili kuwekeza katika maeneo ya kitalii kwa kutoa huduma mbalimbali kama malazi n.k 

No comments