Breaking News

Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa Kukutana na Kufanya Majadiliano na Wadau Kuanzia Sept 23

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatarajia  kukutana na wadau mbalimbali wa vyama vya Siasa ikiwemo Jeshi la Polisi  kwa lengo la kuweka majadiliano ya kuweka  suhulu kati nvyama vya Siasa na Jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Msajili wa vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi alisema nia ya vikao hivyo  ni kuweka mazingira rafiki na maelewano baina ya  vyama Siasa.

Jaji Mtungi amesema kikao cha kwanza Cha wadau kitafanyika Septemba 23 mwaka huu ambapo ofisi hiyo itakutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kwa lengo la kujadili na kupata ufumbuzi juu ya malalamiko yanayotolewa na baadhi ya vyama vya Siasa katika ofisi hiyo.

Sanjali na kikao hicho Jaji Mutungi amesema Septemba 30 ofisi hiyo itaitisha kamati ya Uongozi ya vyama vya Siasa ambapo kikao hicho kitaongozwa na kanuni ya baraza la vyama vya Siasa.

Vilevile amesema kuwa Octoba 13 mwaka huu baraza la vyama siasa litafanya mkutano mkubwa visiwani Zanzibar ambapo utashirikisha wadau mbalimbali wa vyama vya Siasa.

"Mkutano huu utaendeshwa bila ya kuepo upendeleo kwani utaendeshwa na Waziri ambaye anamafungano ya vyama siasa ili kutia fursa kwa vyama vya Siasa kuelezea chagamoto zinazowakaba na kufikia Maridhiano"alisema

Vikao hivi vinakuja ikiwa bado kunamalalamiko ya baadhi ya  wadau wa vyama vya Siasa kushidwa kufanya mikutano yao kwa kueleza Jeshi la Polisi kuwaingilia. 

Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa Kukutana na Kufanya Majadiliano na Wadau Kuanzia Sept 23.

No comments