MTANZANIA ASHINDA TUZO YA VIJANA WENYE USHAWISHI WA MAENDELEO AFRIKA
Mtanzania Steven Magombeka Maarufu Kama Kasampaida ameshinda Tuzo ya Vijana Wenye Ushawishi Barani Afrika katika Tuzo zilizotolewa Usiku wa Kuamkia Leo jijini Accra Nchini Ghana Tuzo Zinazosimamiwa na Uongozi wa Vijana wa Pan African
Tuzo hizi mashuhuri zinawatambua Vijana wajasiriamali bora, wanaharakati, waleta mabadiliko na wafuatiliaji ambao wameonyesha ubora wa kipekee katika nyanja zao Kukiwa na takriban uteuzi wa vijana 5,000 kutoka nchi 52 za Afrika.
Pongezi za dhati kwa Vijana 100 Wenye Ushawishi Zaidi wa 2025! Mafanikio yako bora yanaendelea kutia moyo na kuleta mabadiliko katika bara zima na kwingineko.
Post Comment