Breaking News

PROF LIPUMBA AMTAKA RAIS DKT SAMIA KUKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Lipumba, ametoa ushauri kwa Rais jamhuri ya muungano wa Tanzania, dokta Samia Suluhu Hassan kukaa na Viongozi wa Vyama Vyote vya Siasa nchini kujadili changamoto zilizopo kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.

Akizungumza katika mkutano na wananchi uliofanyika kwenye viwanja vya bakhresa, Manzese leo Aprili 12, 2025 jijini Dar es Salaam Prof. Lipumba amesema kama taifa na ukidhingatia tunaelekea katika uchaguzi mkuu kwa mazingira tulionayo nitoe rai kwa rais samia kuitisha kikao na kukaa na viongozi wote wa vyama vya siasa kwa lengo la kupata mwafaka wa pamoja.

"Wito wangu kwa Rais Samia, aangalie namna ya kukutana na viongozi wa yama vya siasa ili tujadili kwa pamoja matatizo yaliyopo kabla ya kuingia katika Uchaguzi, naamini Mama yetu ni msikivu na katika hili anaweza kulifanyia kazi ipasavyo,". Alisema Prof. Lipumba.

Alisema ikimbukwe kuwa wakati Rais Samia anaingia madarakani wote tuliamini kuwa changamoto zikizojitokeza katika chaguzi zilizopita zingepatiwa ufumbuzi wa haraka lakini mpaka sasa tunajianda kelekea katika uchaguzi mkuu bado baadhi ya changamoto bado azijawahi kupatiwa ufumbuzi.

Alibainisha kuwa licha ya changamoto hizo bado haijafanyiwa kazi, wito wake kwa Rais afanye mchakato wa kukutana na viongozi wa vyama vya siasa wajadiliane Kwa pamoja na kupata njia sahihi ya kuingia katika uchaguzi kila mgombea akiaminj mazingira mazuri yamewekwa ya kushinda.

Prof. Lipumba aliongeza kuwa licha ya changamoto hizo kuelezewa kwa kipindi kirefu ikiwemo mchakato wa kudai Katiba Mpya na Tume Huru kulianza kipindi kirefu hali iliyopelekea Tume ya Jaji Nyalali, Tume ya Kisanga, Tume ya Jaji Warioba zote zilielezea umuhimu wa kuwepo na misingi ya kidemokrasia na kupendekeza yafanyike marekebisho hadi sasa hakuna mabadiliko ya msingi yaliyofanyika.

"Viongozi wa vyama vya siasa mwaka 2014 jijini Dodoma walikaa na Rais wa wakati huo Jakaya Kikwete kujadili mchakato huo na walikubaliana yafanyike mabadiliko madogo na hadi sasa bado mengi hayajafanyiwa kazi". Alisema Prof. Lipumba.

Alisema licha ya madai hayo kutofanyiwa kazi hadi sasa ikiwemo kupata Tume Huru ya Uchaguzi hata marekebisho yaliyofanyika sasa bado wamo baadhi ya wajumbe hawastahili kuwemo katika tume hiyo lakini pamapja na kuwepo kwa changamoto hiyo CUF hatutasusia uchaguzi.

"Hatuwezi kususia uchaguzi wa mwaka huu kwani naamini njia sahihi ni kushiriki uchaguzi huku tukiendelea kushinikiza na kudai madai yetu yafanyiwe kazi kwan CUF bado tunamtambua Rais Samia kuwa ni halali," .Alisema Prof. Lipumba.

Awali akizungumza wakati akimkaribisha mwenyekiti wa chama hicho taifa, Makamu Mwenyekiti CUF, Othuman Dunga, amesema katika mazingira kama haya hatuwezi kupata maridhiano yenye tija kama bado sisi wenyew hatujawa wamoja.

Alisema CUF kwa sasa tutajikita zaidi katika kuhamasisha mabadiliko ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa Tume Huru ya Uchaguzi na wala sio kususia uchaguzi.

"Nitoe msisitizo katika hili kwa watanzania kuwa Uchaguzi Mkuu ni fursa ya kuleta mabadiliko na mabadiliko yanayokea kwenye sanduku la kura hivyo kususia ni sawa na kujikosesha fursa ya kuleta mabadiliko kwa wanachama wetu pamoja na watanzania kwa ujumla,". Alisema bw. Dunga

Katika hatua nyingine makamu mwenyekiti huyo amewataka watanzania na wakerejetwa wa chama hicho kukiunga mkono chama hicho kwa kutoka michango ambayo itasaidia kuwezesha chama kufanikisha kufanya mikutano nchi nzima pamoja na kufanya vizuri katika Uchaguzi Mkuu.