Breaking News

TADED: HAKUNA CHAMA CHENYE UWEZO WA KUZUIA UCHAGUZI MKUU 2025 USIFANYIKE

Dar es salaam - Taasisi ya Demokrasia na Maendeleo Tanzania (TADED) imesema kuwa hakuna chama au taasisi ya kufanya kuzuia uchaguazi Mkuu ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa TADED Chalila Kibuda amesema kuwa kwa mujubu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga kura ni haki ya watanzania hivyo hawezi chama au Taasisi kuwazuia wananchi wasipige kura.

Amesema TADED katika kipindi cha kuelekea uchaguzi kitahakikisha kinahamasisha wananchi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi mkuu katika kusikiliza mikutano ya kampeni kutoka kwa wagombea pamoja na kushiriki kupiga kura.

Amesema katika kampeni hizo kwa wagombea kunadi sera za vyama vyao na sio kukashifiana ambapo hizo kashfa sio kipaumbele kwa wananchi wanaotaka maendeleo kwa viongozi wataowachagua.

"Uchaguzi huu ni haki ya kila mwananchi kushiriki katika kuchagua viongozi wataodumu kwa kipindi cha miaka mitano kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".amesema 

Aidha amesema suala la chaguzi Mkuu kwa katiba hii hakuna chombo chochote kinachoweza kuzuia kutofanyika uchaguzi ambapo hata chama kilichopo madarakani hakiwezi kufanya hivyo.

Hata hivyo katika maandalizi hayo yamefanyika vizuri ikiwemo wananchi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura nchi nzima.

Kibuda amesema chama fulani kinasema No Reform No election ni jambo ambalo haiwezekani kuleta katikati ya zoezi hilo kuanza.

Hata hivyo tangu kufanyika uchaguzi 2020 katika kipindi hicho chama hichi kilikuwa nafasi ya kufanya juu ya kuliendea jambo la uchaguzi na serikali ikachukua hatua.

Hata hivyo Serikali ya awamu ya sita chini Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuweka utulivu wa Siasa amefanya mambo pamoja na kuwa na maridhiano ya kuruhusu mikutano kufanyika ambapo vyama vinaendelea kufanya mikutano bila vikwazo.

Aidha katika mazingira tulionayo nchi iko tulivu kabisa kila mwananchi anaendelea kufanya maisha yake hii inaonyeesha amani ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na vyombo vyake kuendelea kuhudimia wananchi wake.

Amesema nchi iko salama na kufanya mataifa mbalimbali kuwekeza kwa kigezo kuwa na siasa salama (political Stability).

Katika maendeleo nchi chini Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea kutekeleza miradi yote ikiwemo bwawa la umeme la Nyerere ambapo hadi sasa umekamilika ,huku ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR unaendelea kuanzia Dodoma hadi Mwanza.

Katika sekta ya Utalii idadi ya watalii inaongezeka hiyo inatokana na serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kutengeneza filam ya Royal Tour kwa ajili kutangaza utalii.

Amesema nchi imeendelea kujiimarisha katika mahusiano ya kimataifa kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kufanya ziara ambapo ndio matokeo yanayooneka katika uwekezaji nchini.

Katika mikakati iliyojiwekekea Taasisi ni pamoja na kufanya makongamano nchi nzima kwa kushirisha wasanii mbalimbali ambapo mazungumzo yao yanaendelea kufanyika na hatuwezi kuyatoa kwenye vyombo vya habari pamoja na kukutana viongozi wa wa dini katika kilele cha kampeni kwa viongozi hao kutoa ujumbe kuhusiana na uchaguzi.