Viongozi wa Dini Waishauri Serikali, Jamii
Viongozi wa dini hapa nchini wameisisitiza serikali kuimarisha uchumi kwa wananchi wake ili kuwafanya wanufaike na rasilimali zilizopo.
Akizungumza jijiniDar es salaam Mufti wa Tanzania Abubakari Zuberi alisema umoja wa viongozi wa dini umekuwa ukisisitiza jamii kuzingatia amani, umoja na maadili mema kwa lengo la kusaidia ukuaji wa uchumi kwa Watanzania.
Alisema kuwa viongozi wa kiroho wamekua na utamaduni wa kukutana mara kwa mara kujadili mahusiano mazuri kati ya viongozi wa dini na serikali nakutoa mwelekeo mzuri kwa waumini wake ili kuendelea kuilinda amani.
Akizungumzia kuhusu viongozi wa dini ya kiislam wakiwemo Mashekhe wa uamsho waliopo mahabusu Mufti Zuberi ameziomba mamlaka zinazohusika ikiwemo Mahakama kuu na Ofisi ya Mwandesha mashtaka mkuu wa serikali(DPP) kusikiliza haraka kesi zao nakwamba wale watakaobainika kuwa na makosa sheria ishike mkondo wake na wale wasiokuwa na makosa waachiwe huru.
Kwa upande wa Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania( kKKT) Dr. Alex Malasusa alisema kuwa watoto wengi wamekuwa wakilelewa katika maadili mabovu hali inayochangia kuwepo kwa wimbi kubwa la watoto wa mtaani.
Dr.Malasusa alisema kuwa wazazi wengi wameacha kulea vizuri watoto wao kutokana na kukimbizana na shughuli za kiuchumi nakuwataka wazazi wawajibike ipasavyo katika malezi ya maadili kwa watoto.
"Kila mtu anawajibu wa kulea mtoto, ndiyo maana watoto wengi hawana maadili mazuri kutokana na wazazi wengi kuwaacha peke yao wajilee, tunapaswa kumjenga mtoto kimaadili na sio kumpa chakula, mavazi na matibabu pekee" alisema Askofu Dr.Malasusa.
Nae Askofu Mkuu wa elimu kutoka kanisa la Kipentekoste Petter Konki alisema kuwa endapo watapata nafasi yakuonana na Rais Samia Suluhu Hassan watamuomba ashughulikie hali ya mfumuko wa bei kwani mlaji wa chini ni mtanzania ambaye anamaisha ya kawaida kiuchumi.
Askofu Konki ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja wa makanisa ya kipentekoste nchini(CPCTaliendelea kusema kuwa serikali iwalinde viongozi wastaafu ikiwemo wale walio ondoka duniani na wale walio hai kwa kuwachukulia hatua wale wote wanaotumia maneno ya kukashifu viongozi hao.
"Tunaona viongozi wetu wastaafu wanakashifiwa wengine huku wengine wameshatangulia mbele za haki wengine bado wapo lakini kuna maneno yamekua yakitumika dhidi yao siyo mazuri mfano kuna neno la "mwendazake" ndo linatumiwa sana sasa hivi naomba serikali iwalinde viongozi wetu wastaafu" alisema Askofu Konki.
Post Comment
No comments