Wadau wa Kupinga Ukatili wa Mtoto Waishauri Serikali, Jamii
Kuelekea maazimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambayo huazimishwa juni 16 kila mwaka wadau wamejitikeza nakuiomba jwmii kuacha tabia ya kuficha watoto wenye ulemavu kwani wanahaki sawa wengine.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa sheria na Haki za Binadamu kutoka shirika la Buldining Inclusive Society Tanzania Organization (BISTO) aliema kuwa watoto wanakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutumikishwa kazi za ndani na zile za kuzalisha kipato.
Alisema kuwa watoto wenye ulemavu wamekua wakikosa haki mbalimbaliza za kibinadamu ikiwemo kukosa elimu pamoja na kufichwa ndani huku akiiomba jamii itoe taarifa kwa mamlaka zinazohusika pindi wanapogundua kuna mtoto amefichwa.
"Ndugu zangu watoto wengi wanatumikishwa katika kazi za kuingiza kipato kama ombaomba tunaikumbusha jamii kuacha vitendo hivi siyo vizuri na vinatakiwa kukemewa kwa nguvu zote" alisema Nzige.
Kwa upande wake Bi Sophia Komba Mkurugenzi mkuu wa Kituo cha Kupinga unyanyasaji wa kijinsia CAGBA na mwenyekiti wa TAANET alisema kupunguzwa kwa kodi kwenye bidhaa za vinywaji vikali ( Pombe) inaweza kuchangia vitendo vya unyanyasaji kwa watoto ikiwemo ubakaji.
Alisema kwamba serikali iangalie kwa upana suala hilo kwani linaweza kusababisha matatizo makubwa kwa jamii ikiwemo kuongezeka kwa walemavu kutokana na ajali zitokanazo na madaereva bodaboda waliolewa.
"Kitendo cha kupunguza kodi kilichofanywa na serikali kupunguza kodi katika vileo kinaweza kusababisha kuongezeka kwa ajali nashauri kuangalia upya swala hili" bi. Komba.
No comments