Breaking News

SEMU: WANAWAKE TUUNGANE KUDAI HAKI NA KUPIGANIA MAGEUZI NCHINI

Na Neema Mpaka - Chama Cha ACT wazalendo kimewataka wanawake kote nchini kuungana kwa pamoja kudai mageuzi na kupigania haki zao, pamoja na kupinga mikopo umiza na unyonyaji mwingine bila kujali tofauti ya vyama vyao.

Akizungumza Leo jiji dare es salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyoandaliwa na ngome ya wanawake ya ACT wazalendo kiongozi wa chama Cha ACT wazalendo Ndugu Doroth Semu amesema mikopo mingi inatolewa kwa upendeleo, na inaishia kwenda kwenye vikundi ambavyo havifanyi Kazi husika.
"Wakati wote tumekuwa tukiiambia
 serikali ya chama Cha mapinduzi kwamba mikopo humiza inauwa biashara za akina mama,inauwa nguvu za wajasiliamali na tuliweka mfumo kuwe na mikopo ya almashauri isiyokuwa na riba" Amesema Bi Semu.

Aidha amesema fedha hizo za mikopo kunatakiwa kuwekwe 
 utaratibu Bora ambao utaondoa mambo ya riba kubwa na ambao utamwezesha mwanamke mjasiliamali mdogo mdogo, kijana na watu wenye ulemavu kupata mikopo hiyo kwa urahisi, kwa haki ili waweze kurudisha mikopo hiyo.

"Tunaona serikali ya chama Cha mapinduzi imehamishia mikopo hii kwenye mabenki wale ni wafanyabiashara ni lazima wananchi wakitaka kuomba mikopo watakutana na vigezo vya kibenki" Amesema Doroth.
Amesema wataendelea kupaza sauti na kuhakikisha kwamba wanawaondoa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwenye lindi la mikopo umiza, mikopo yenye riba kubwa, mikopo ambayo imeenda kuuwa, kudhalilisha lakini pia imewafanya wanawake kuwa omba omba na wengine kukimbia maeneo wanayoishi.

Wakati huo huo kiongozi huyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwani ni fursa ya kwenda kuhakiki majina Yao, lakini pia kwa wale wananchi waliotimiza miaka 18 na ambao walikuwa hawajajiandikisha kabisa kujitokeza kujiandikisha ili kuweza kushiriki katika chaguzi zijazo.








No comments