Breaking News

Dr. Chamuriho Awatoa Hofu Wadau wa Usafirishaji Nchini

Taasisi zinazo simamia sekta ya usafirishaji nchini zimetakiwa kuacha urasimu nakutakiwa kuwa na ushirikino na wadau wa sekta ya usafirishaji ili kutatua changamoto  wanazokutana nazo wadau hao wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza jijini Dar es salaam Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk. Leonard Chamuriho wakati akifunga mkutano wa wadau wa usafiri na usafirishaji kuhusu fursa za kiuchumi pamoja na changamoto zilizopo ambapo baadhi ya wadau hao wamezilalamikia baadhi ya taasisi hizo kuwa hazina ushirikiano na wadau hao.

Dk. Chamuriho alisema kuwa kuna baadhi ya changamoto zinazowakumba wadau wa usafirishaji ambazo zinaweza kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo ngazi ya chini na sio kusubiri hadi viongozi wa mamlaka za juu waitishe mkutano kusikiliza kero za wadau hao.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na Taasisi ya Sekta binafsi nchini TPSF ulikua na lengo la kusikiliza changamoto zinazo wakabili wadau hao na kuzichakata  kabla ya kuzifikisha kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la  Biashara utakaofanyika Juni 26 mwaka huu, ambapo mgeni rasmi atakua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Wadau hao wamelalamikia baadhi ya  faini zinazotozwa na mamlaka za usafirishaji ikiwemo mamlaka ya usimamizi wa vyombo vya usafiri ardhini  (Latra), Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani pamoja na mamlaka ya usimamizi wa barabara nchini (TANROADS) kwa makosa mbalimbali ya barabarani kama vile kosa la mwendo kasi ambapo wamedai faini zao zimekua zikikinzana kwa mujibu wa sheria hivyo suala hilo litazamwe upya.

Pia wadau hao wakiwemo chama cha wamiliki wa mabasi ((TABOA) wamelalamikia mfumo wa kukata tiketi  mtandaoni (E-TICKET) kwamba baadhi ya mawakala wanaotoa huduma hiyo wumekuwa wunasababisha  usumbufu mkubwa kwa abiria.

Kwa upande wake mwenyekiti wa TPSF, Angelina Ngalula alisema kuwa sekta binafsi imechangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta maendeleo kwa Taifa hivyo anashukuru serikali ya awamu ya sita imetoa kipau mbele zaidi katika sekta binafsi.
Alisema kuwa kwa sasa sekta binafsi inaendelea kuchangamkia fursa mbalimbali za biashara nakwamba kutokana na serikali kuamua kuchukua hatua ya kuondoa baadhi ya vikwazo ikiwemo utitiri wa kodi na faini mbalimbali wanaimani watapiga hatua kubwa zaidi katika kuchochea maendeleo ya Taifa.

No comments