Breaking News

TGNP Mtandao Yawajengea Uwezo Wanafunzi Wasichana Kutoka Vyuo Vikuu 10 Jijini Dar.

Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Bi. Liliani Liundi akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike juu ua ushiriki wamwanamke katika uongozi kutoka vyuo vikuu 10 jijini Dar es salaam.

TGNP Mtandao imeendesha mafunzo ya uongozi maalumu kwa wanafunzi wasichana kutoka vyuo vya elimu ya juu kwa lengo la kuwahamasisha na kuwajengea uwezo vijana wa kike kuwezesha kushiriki katika kuwania nafasi za uongozi kuanzia ngazi ya vyuoni na nje ya vyuo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo jijini dar es salaam, mkurugenzi wa TGNP Mtandao Bi. Liliani Liundi alisema mafunzo hayo ya sku nne yatajikita zaidi katika kuwanoa na kuwapa ujasiri wa kuthubutu kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za maamuzi kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Alisema kwa mujibu wa takwimu za Interpaliamentary Union (IPU) ya mwaka 2017 zinaonyesha kuwa ushiriki wa wanawake katika uongozi katika ukanda wa afrika mashariki Tanzania imekuwa mmoja ya nchi zinazofanya vizuri katika ushiriki wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi.
 “Tanzania ni moja ya nchi zinayofanya vizuri katika ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi kwa kushika nafasi ya 2 kwa nchi za afrika ya mashariki na nafasi ya 25 duniani kwa kuwa na asilimia 36 wa wabunge” Alisema Bi Liundi.

Bi liundi aliongeza ikiwa bado atujafikia 50/50 pamoja na kwa mara ya kwanza tangu uhuru tumeweza kuwa na mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa rais Mama Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge la 10 Mhe Anna Makinda pamoja na Naibu spika katika bunge la 11 Mhe Dkt Tulia Akson bado juhudi zaidi zinahitajika kuongeza nafasi za wanawake katika ngazi za maamuzi.

Jumla ya wanafunzi wa kike kutoka katika vyo vya elimu ya juu zaidi ya 10 kutoka dar es salaam, Arusha na mkoani Morogoro wameshiki mafunzo hayo ya siku nne.


 Baadhi ya washiriki mafunzo ya siku nne  kutoka katika vyuo vya elimu ya juu zaidi ya 10 kutoka dar es salaam, Arusha na mkoani Morogoro jijini dar es salaam

No comments