RC CHALAMILA KILA MTU ALIPE KODI KULINGANA NA KIPATO CHAKE
# Amshukuru Rais Dkt Samia kwa namna anavyoendelea kuimarisha TRA
# Asema Kodi inayolipwa inaonekana hususani DSM miradi mingi ya maendeleo inatekelezwa kwa mfano mradi wa ujenzi wa barabara za mwendokasi.
Dar es salaam - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila ametaka kila mtu kulipa kodi kulingana na kipato chake kwa maendeleo ya taifa.
Akizungumza katika hafla ya ugawaji tuzo kwa walipa kodi wa bora Mkoa Dar es salaamvvv iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika ukumbi wa Mlimani City amesema kodi ni jambo la msingi na lazima hivyo ni vema jamii ikatambua umuhimu wa kila mmoja kulipa kodi kulingana na kipato chake ambapo ameitaka TRA kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa umma
"Kodi ni jambo la msingi na lazima hivyo ni vema jamii ikatambua umuhimu wa kila mmoja kulipa kodi kulingana na kipato chake nitoe rai TRA kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa umma ili kodi ikusanywe bila manung'uniko watu walipe kwa hiari". Alisema RC Chalamila
Alisema Rais Dkt. Samia Hassan amekuwa akichukua hatua za makusudi kuendelea kuimarisha Mamlaka ya Mapato Tanzania sasa kodi imekuwa ikikusanywa bila manung'uniko lakini pia amekuwa akitoa pesa nyingi kuendeleza miradi inayotekelezwa katika Mkoa wa Dar es Salaam "Kodi inayolipwa inaonekana".
katika hatua nyingine RC Chalamila amewataka watanzania kuwa na utaratibu wa kudai risiti kila wanapofanya manunuzi, kujiepusha na vitendo vya ukwepaji kodi, wafanyabiashara walipe kodi kwa hiari bila shuruti.
Kwa upande wa Kamishna Mkuu wa TRA Bwana Yusufu Mwenda amesema mkoa wa Dar es salaam unachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la Taifa hivyo TRA imejipanga kuhakikisha kuwa inaendelea kupambana na biashara za magendo, kuendeleza utulivu wa kibiashara pamoja na kuwekeza kwa watumishi wake sambamba na kuweka mazingira rafiki kwa mlipa kodi
No comments