Breaking News

Waziri Kakunda: Hakuna Nchi Iliyoendelea Kufikia Viwanda Vikubwa Bila Kuhimiza Uendelezaji Viwanda Vidogodogo.

Image result for waziri kakunda
Waziri Kakunda amesema kuwa bila kuhimiza uendelezaji viwanda vidogo vidogo ni vigumu nchi yeyote duniani kufikia sekta yta viwanda vyenye tija kiuchumi kwa nchi.
“Hakuna nchi iliyofanikiwa kiviwanda  bila ya kuanza kusisitiza na kuhimiza kuviendeleza na viwanda vidogodogo,SIDO ndio baba ya viwanda na mama viwanda hapa nchini kwa hatua yake ya kuanza kumiliki viwanda vidogo”Amesema Waziri Kakunda.

Amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inasapoti  viwanda vidogovidogo lengo likiwa kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda huku akisistiza,wananchi wakiendelea kusapoti  Sido itasababisha uchumi kukua.

Ameongeza kuwa viwanda vidovidogo vikiendelea kuimarika vitapelekea kukuza uchumi wa n chi kwani bila sekta hii nyingine haziwezi kupiga hatua kimaendeleo.
Katika hatua nyingine Waziri Kakunda ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha inaendelea na  sekta ya viwanda ikiwemo uongezaji ufanisi wa Sido taifa lipige.

Kwa Upande wake  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la kuhudumia wenye viwanda vidogo(SIDO),Profesa Elifas Bisanda amesema bodi hiyo itahakikisha wanaiweka Sido kwenye ramani ya nzuri ili kuvisaidia  na  kuviinua  viwanda vidogodogo.

No comments