Breaking News

RC CHALAMILA ATANGAZA RASMI KUANZA UUZWAJI WA VIWANJA MABWEPANDE - KINONDONI

Dar es salaam - Kufuatia maelekezo aliyoyatoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwataka waliovamia na kujenga kwenye eneo linalomilikiwa na shirika la maendeleo Dar es Salaam (DDC) lililopo Mabwepande kuuziwa viwanja hivyo kwa gharama nafuu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila kwa kushirikiana na shirika hilo pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni ametangaza rasmi rasmi kuanza kuuza viwanja katika eneo hilo

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 8, 2025 eneo la Mabwepande akiwa ameambatana Katibu Tawala wa Mkoa Dkt. Toba Nguvila, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, viongozi wa DDC pamoja na wataalamu wa ardhi kutoka Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni, RC Chalamila amesema eneo hilo lenye viwanja zaidi ya 2274 vyenye ukubwa tofauti tofauti ambavyo baadhi vilivamiwa na vingine havijavamiwa vitaanza kuuzwa rasmi. 
Aidha RC Chalamila amesema viwanja hivyo vitaanza kuuzwa kuanzia wiki ijayo kwa wananchi waliovamia kwa miaka mingi na bado wapo katika eneo hilo watauziwa kwa gharama ya shilingi elfu tatu kwa mita ya mraba wakati wengine watakaohitaji viwanja watauziwa kwa shilingi elfu 15,000, 17,000 na 20,000 kwa mita ya mraba kulingana na matumizi yake kama makazi, biashara au matumizi mengine

Katika hatua nyingine RC Chalamila amewaka wananchi watakaonunua viwanja hivyo kuwa Rais Dkt Samia ameshapeleka huduma muhimu za kijamii kwenye eneo hilo ikiwemo umeme na maji na kwamba barabara ipo kwenye mpango wa ujenzi wa kiwango cha lami kupitia TANROAD

Kwa upande wa Afisa mipango miji Manispaa ya Kinondoni Arkadius Haule amewahakikishia wananchi kuwa viwanja hivyo vyote vimepimwa na vitauzwa kwa kuzingatia uhitaji wa mnunuzi huku Ali Mirambo Meneja Mkuu wa DDC akiwahakikishia wananchi kuwa eneo hilo ni mali ya shirika hilo hivyo wanauziwa na mmiliki halisi


No comments