Breaking News

Prof Lipumba Amtangaza Khalifa Suleman Khalifa Kuwa Katibu Mkuu CUF Taifa.

Chama cha wananchi CUF upande wa mwenyekiti anaetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini Prof Ibrahim Lipumba kimeteua bw Khalifa Suleman khalifa kuwa katibu mkuu wa chama hicho a kuchukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad. 

Akimtangaza mapema leo makao makuu ya chama hicho buguruni jijini Dar es Salaam Prof limbumba alisema kikao cha baraza kuu kilicho kaa mapema leo jijini Dar es Salaam kwa kauli moja wamemteua bw Khalifa Kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama hicho. 

Kikao hicho pia kimewateua Manaibu wakuu wawili ambao kwa upande wa Tanzania bara ameteuliwa mhe. Magdalena Sakaya na upande wa Zanzibar ameteuliwa bw. Faki Sulemani khatib. 

No comments