Breaking News

MUSIBA Amtaka Mhe Mbowe kuacha kutafuta Huruma Kwa Wananchi

Mwanaharakati huru na mkurugenzi wa CZI bw, Cyprian Musiba ametaka mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Mhe. Freeman Mbowe kuacha kutafuta huruma ya wanachi na badala yake ajikite kuangalia namna ya kutatua changamoto zilizopo ktk chama chake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Bw Musiba alisema kitendo cha mwenyekiti huyo kukimbilia katika vyombo vya habari na kuanza kulalamika juu ya hatua iliyochukuliwa na mahakama ya kumweka ndani kuwa ni kutokana na kuizarau mahakama.

"Nimtamke mhe mbowe kuacha kutafuta huruma kwa wananchi kutokana na yeye mwenyewe kudharau mahakama kupitia wakili wake ambae walitoka taarifa kuwa alikuwa amesafiri kwemda nje ya nchi kutokana na kuumwa jambo lilopelekea mahakama kimfutia dhamana"Alisema bw Musiba. 

Alisema yeye kama mwanaharakati huru na mfuasi wa rais John Pombe Magufuli atokaa kimya kila atakapo ona vitendo ambavyo ni hujuma za mkumzoofisha na Kumchafua mhe rais. 

"Watanzania tuendelee kumpa ushirikiano rais Magufuli katika kipindi chote cha utendaji wake kwani ni mzalendo wa kweli na amedhamilia kuwaletea maendeleo watanzania wote bila kujali Itikadi zao" Aliongeza bw Musiba. 

No comments