Mgogoro Wa Uongozi Ndani ya CUF Wachukua Sura Mpya
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjE6eXKtDYRXY9U_cWSD5EUB48U1rZTKo6yL_OB93HS_YlMC1YsjtUAfsRHMNsnKeO6PcthheJ6iLPpLwfmJ5iLWtKLFMZZPVbOGRXq1YQ5dLNl0I4jITnd2QP_NN-ZFIQYze_tX9ApOaQh/s640/IMG_20190309_120045.jpg)
Mgogoro wa Uongozi ndani ya chama cha wananchi CUF umeendelea kuchukua sura mpya kufatia upande unaongozwa na katibu mkuu mhe Seif Sharif Hamad kusema kinachofanywa na upande wa mwenyekiti anaetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa prof ibrahim lipumba kuwa ni mwendelezo wa hujuma na kukahidi maamuzi ya mahakama.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam Naibu katibu mkuu wa chama hicho Bara Bw. Joran Bashange alisema anasikitishwa na hujuma ambazo zimekuwa zikiendelea kufanywa na prof lipumba na pamoja na Taasisi nyingine za kiserikali ambazo ni wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) pamoja na msajili wa vyama vya siasa nchini.
"Kumekuwepo na mipango ya kuendelea kukihujumu chama licha ya mahakama kutoa hukumu kwa baadhi ya mashauri likiwemo shauri la Bodi ya Wadhamini wa Chama hicho na amri ya zuio kuitisha mkutano mkuu wa taifa mpaka hapo shauri la msingi no 84/2018 litakaposilizwa na kutolewa uamuzi" Alisema Bw. Bashange.
Alisema pamoja na maamuzi haya ambayo yametolewa na mahakama lakini mwenyekiti anaetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa prof ibrahim lipumba amekuwa akipuuza na kuendelea na maandalizi ya mkutano mkuu ambao wamepangwa kufanyika tarehe 12 hadi 15 jijini Dar es Salaam.
Aidha bw. Bashange aliongeza kuwa chama cha wananchi CUF kimekuwa kikiheshimu utii wa sheria katika kipindi chote cha mgogoro wao ila kwa mambo na mipango ambayo imekuwa ikifanywa na Prof Ibrahim Lipumba za kuingilia uhuru wa mahakama tayali tumemwandikia IGP wa polisi nchini Simon Sirro kumtaadhalisha juu ya hatua hiyo.
"Kufatia maamuzi ya kukiuka uhuru wa mahakama tayali tumemwandikia barua IGP wa jeshi la polisi nchini Simon Sirro, Jaji mkuu, Jaji Kiongozi, Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, RPC Ilala pamoja na OCD kituo cha polisi buguruni" Alisema bw Bashange
Bw. Bashange pia ametoa wito wanachama wa CUF mkoa wa dar es salaam na walinzi wote wa chama kufanya kila wawezalo kuakikisha kuwa wanakilinda chama kwa gharama yeyote.
No comments