Mhe. Majaliwa kufungua kongamano la kitaifa kutokomeza ukatili dhidi wanawake na Watoto
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgcCxMS_iDrPE8NBdyYIPmWwFTyeu-8DLJbGHH7vhEDvvOMIh0QAv4lXC4IfsZYOAmKIyekWJnbuVTZg9IGud4FvE64GC4QzH0WA8yjFrz-D2341RdQMHOKZChgD7ANC8pBPBtvYyR6yWzQ/s640/IMG_20190313_103420.jpg)
Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF chini ya udhamini wa ubalozi wa Uswisi kwa kushirikiana na shirika la C SEMA na chuo kikuu kishiriki cha elimu (DUCE) wameandaa kongamano kitaifa la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto litakalofanyika tarehe 22 na 23 mwezi huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam mkurugenzi wa CDF bw. Koshuma mtengeti alisema mgeni rasmi katika ufunguzi wa kongamano hilo atanatarajiwa kuwa Waziri mkuu mhe Kasimu Majaliwa ambapo washiri wapata fursa ya kujadili hali ya ujatili dhidi ya wanawake na watoto na namna nini kifanyike kutokomeza vitendo ivyo.
"Kongamano hilo la siku mbili ambalo litawakutanisha washiriki zaidi ya mia sita kujadiliana namna na nini kifanyike kutokomoza ukatili dhidi ya wanawake na watoto" Alisema Bw. Mtengeti.
Alisema kupitia kongamano hilo viongozi wa kitaifa, watafiti, Asasi za kiraia, Wanataaluma, Viongozi wa Dini, wanaharakati wa haki za binadamu pamoja na wadau wa maendeleo watapata fursa ya kujadili hali ya ukatili na namna ya kuimarisha mikakati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Aidha bw Mtengeti alibainisha kuwa katika kongamano hilo mada kuu sita zitawasilishwa ambazo ni hali ya ukatili kwa watoto katika familia na mashuleni, ukatili wa kijinsia na unyanyasaji, mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni.
Amezitaja nyingine kuwa ni Ukeketaji, malezi katika ulimwengu wa kisasa, ukatili wa kingono katika taasisi za elimu ya juu, utatili dhidi ya watoto kwenye mitandao na namna ya kuwapatia msaada waanga wa vitendo vya ukatili.
No comments