Panya Wamkera Mkuu Wa Mkoa, Atoa Maagizo Kwa Viongozi
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbwanga Dk. Khalfan Haule kuhakikisha
anatafuta dawa ya kuulia panya wakiwa mashambani ili kuokoa miti kutokana na
uchomaji wa misitu kwasababu ya uwindaji wa panya.
Amesema kuwa ameisikia changamoto
hiyo ya uchomaji wa misitu kwasababu ya uwindaji wa panya kutoka kwa vijana
mbalimbali wanaojishughulisha na mashamba ya upandaji miti pamoja na taarifa
iliyosomwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga juu ya
changamoto za kuendeleza misitu.
“DC tafuta dawa ya panya, wauliwe
huko mashambani, ili panya wasiwepo na miti iokoke, mbona hamshangilii? Hawa
panya tutawaua kwa sumu huko mashambani wasiwe chanzo cha mioto ambayo mnachoma
huko kuwatafuta hawa panya ili wafie huko huko mashimoni msiwapate,”
alisisitiza.
Agizo hilo amelitoa katika muendelezo
wa kampeni ya upandaji miti mijini na vijijini katika Kijiji cha Mpwapwa, kata
ya Mpwapwa, Wilayani Sumbwanga baada ya kuwauliza wananchi wa Kijiji hicho juu
ya changamoto aliyoisikia ya uchomaji wa moto misitu kutokana na kuwinda panya,
japo wananchi walikataa.
Pia katika kuongezea hilo alimuagiza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kuhakikisha anasimamia sheria
ya hifadhi ya mazingira na kuwawajibisha wote wanaohusika na uharibifu wa
mazingira.
Nae akisoma taarifa Mkurugenzi wa H/W
ya Sumbawanga Nyangi Msemakweli alibainisha kuwa miongoni mwa changamoto ni
muitikio mdogo wa uhifadhi wa mazingira pamoja na mila na tamaduni za wananchi
za uwindaji wa panya hali inayosababisha uchomaji wa misitu wakati wa kiangazi.
“Changamoto nyingine ni baadhi ya
viongozi wa serikali ya Kijiji kujihusisha na uuzajia wa maeneo yaliyotengwa
kwaajili ya hifadhi ya Kijiji na usimamizi mdogo wa sheria ndogo za vijiji
katika utunzaji wa misitu,” Alimalizia.
Mmoja wa vijana wanaojishughulisha na
upandaji kiti wa kibiashara Julius Magaga alimweleza Mh. Wangabo kuwa chnagmoto
inayowakatisha tamaa vijana wengi ni kutokana na uwindaji wa panya uliokithiri
na kusababisha hasara katika misitu.
Kwa msimu wa 2017/2018 hadi 30/1/2018
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbwanga imepanda miti 830,527 ambayo ni sawa na
55.4% na ina misitu 92 yenye ukubwa wa jumla ya Hekta 49,179.6. Huku Mh.
Wangabo akigawa miche 850 kwa kaya 850 za Kijiji cha Mpwapwa, Wilayani Sumbawanga.
No comments