Breaking News

Majina Ya Wanachama Wa Cuf Waliotumbuliwa Wilaya ya Ilala.

Kamati ya utendaji (w) ya ILALA iliyo kutana Tarehe 20/01/2018 pamoja na mambo mengine iliyojadili na kuchukua hatua za KINIDHAMU kwa viongozi wa chama cha wananchi [CUF] Wilaya ya ILALA.

Kwa mujibu wa katiba ya Cuf Ibara ya 33(1) inatoa mamlaka kwa kamati ya Utendaji ya wilaya kumsimamisha uongozi Mwenyekiti wa Wilaya na hivyo kamati ya utendaji imefuata muongozo sahihi wa katiba na kuchukua hatua kwa viongozi wafuatao,

Viongozi waliochukuliwa hatua ni BAKAR SHABAN SHINGO amesimamishwa UENYEKITI wa wilaya na Ndugu OMARY ALLY MWARABU amepigiwa kura ya kutokuwa na imani nae kwa makosa ya KUHUJUMU chama wilaya ya Ilala.

Kwa mujibu wa Katiba ya Cuf Ibara ya 73(1) inatoa mamlaka ya kumsimamisha katibu au kumfukuza uongozi katibu wa wilaya ni kikao cha kamati ya utendaji Taifa hivyo kikao cha kamati ya utendaji wilaya ya Ilala kimepeleka pendekezo la kufukuzwa katika nafasi ya ukatibu wa wilaya .

Kamati ya utendaji wilaya pia imempendekeza Mhe MUSSA HEMED MFAUME kuwa kaimu MWENYEKITI wa wilaya ya ILALA na Ndugu ALLY HUSSEN MANINGI kuwa kaimu katibu wa wilaya ya Ilala mpaka kamati ya utendaji Taifa itakapo jubu pendezeko la kamati ya utendaji wilaya ya Ilala.

Siku ya tarehe 9/2/2018 Kaimu MWENYEKITI wa wilaya ya Ilala kwa kutumia Ibara ya 70(6)amefanya mabadiliko ya vitengo vya chama wilaya ya Ilala kama ifuatavyo.

1 ALLY H MANINGI kitengo cha mipango na uchaguzi nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na ABOUBAKARI KITOGO.

20 NURU H OTTOW Kitengo cha fedha nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Ndugu SAFINA MGUMBA.

3 ATHUMAN H SAID Kitengo cha ulinzi na usalama nafasi hiyo alikuwa akishikilia awali.

4 ABUBAKAR FAMBO kitengo cha sheria na haki za binadamu nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Ndugu MOHAMED MLUYA .

5 DR, SAID BADRI MATASA Kitengo cha Habari, uenezi na umma nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na RUKIA MOHAMED.
6.MOHAMED HALFANI MZALA kitengo cha siasa nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na MCHUNGAJI KARISTUS.
Mwenyekiti wa wa wilaya anawaomba viongozi wote na wanachama wa wilayua ya Ilala kutoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi hao wateule wa chama.

Kwa sasa viongozi wote wa wilaya ya Ilala wameamua kupiga kambi jimbo la kinondoni kuhakikisha chama kinashinda kwa ushindi mnono, wanachama na wapenzi wa chama tuungane kwenye jimbo hilo.\
HAKI SWA KWA WOTE !!
Imetoliwa na
ALLY HUSSEN MANINGI
KAIMU KATIBU WA (W) ILALA
0714 850095

No comments