Jaji Mkuu Aionya Serikali
Jaji Mkuu nchini
Kenya David Maraga, ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume
cha Sheria na Katiba ya nchi hiyo katika kukabiliana na upinzani.
Jaji Maraga
ametoa kauli hiyo ikiwa imepita masaa kadhaa tokea kufukuzwa kwa mwanasheria
maarufu ambaye alikuwa miongoni mwa watu walioshuhudia kuapishwa Raila Odinga
katika uwanja wa ‘Uhuru Park’ kufukuzwa nchini humo na kupelekwa Canada.
Katika ukurasa wake
wa Twitter Jaji Maraga amesema malalamiko yaliyopelekwa Mahakamani yalikuwa
wazi na majukumu ya kufanyia maamuzi yalikuwa ya Mahakama kutokana na kwamba
ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila mmoja pamoja na serikali yenyewe.
Jaji huyo ametoa tamko
hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha
serikali ya Kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama.
No comments